Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KIBALI CHA MAISHA
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Maandiko haya ni bure wala isijesemwa yalitolewa ili nijipatie faida ya Fedha au faida yoyote Ile. Yalipatikana Bure nami nitayatoa bure, ili kila asomaye ayapate Kwa gharama Sawa na bure hata Kama isipokuwa bure kabisa. Nayo yawe busara Kwa walio na busara, yawe Kheri Kwa waitakayo Kheri, nao wapendao hekima waipate.
Haya nayo nilikuandikia, basi yashike maneno yangu,
Atukuzwe yeye aishiye sirini, huyo mwenye nguvu ndiye Mungu wa Baba yako.
Yeye aliyenipa kibali cha kukuandikia haya, basi na akupe kibali cha kusoma na kuelewa.
Haya Soma;
Nawe utakapokuwa katika Dhoruba, utakapopita katika njia ngumu, na kama hukujipitisha Ila maisha yalikupeleka huko, maisha yakakupitisha katika Tufani mpaka ukabaki njia panda usijue uchukue njia ipi, ukawa Kama mtu aliyechanganyikiwa, ukajiona unaweweseka, basi usisahau haya nikuambiayo, wala sitaki usijue mambo haya.
Nayo maisha yakikupitisha katika njia ya Maradhi ya kutisha, ama katika vita vikubwa na watoto uliowazaa, ama katika vita na Mkeo au mumeo, au vita na waliokuleta Duniani naam ndio wazazi wako, ama maisha yakakupitisha katika ulemavu ingawaje ulizaliwa ukiwa mzima, ama maisha yakakupitisha katika ufungwa; ukatiwa jela Kwa makosa ya kusingiziwa, au tufani yoyote Ile basi usiwe na hofu, wala usije ukakufuru ukasema maisha yafaa nini, wala usijesema Mungu Hana msaada kwako maana hiyo njia uliyopitishwa niya mpito, na wala haitadumu ingawaje yaonekana ni njia yakudumu.
Mshukuru Mungu Kwa yote hayo Kwa maana hivyo ndivyo utakavyoshinda.
Au Kama wewe ndio ulijipitisha katika njia hizo ngumu, Kwa kujua au Kwa kutokujua, Kwa makusudi au Kwa kutokukusudia, basi usijute Sana wala usijilaumu, wala usijiadhibu Nafsi yako, Bali irejeshe Nafsi yako Kwa Mungu wako, nawe uungame Kwa dhati, wala usitarajie kuondolewa uliyojipitisha Kwa maana huenda hayo ndio malipo yako kwayo. Bali uombe tuu msamaha Kwa maana Msamaha ni muhimu kuliko maumivu uyapitiayo.
Haya Sikia;
Huwezi fanya lolote kwenye maisha pasipo kibali, tena huwezi miliki lolote bila ya Kibali.
Vipo vibali vya Aina nyingi lakini Leo hii ambayo kwako Leo yako ni siku utakayosoma au kusomewa au kusikia habari hii au ifananayo na hii.
1. Kibali kibali cha kudumu
2. Kibali cha muda mfupi.
1. Kibali cha kudumu
Kibali cha kudumu ni kibali ambacho mtu au kiumbe hupewa Kwa muda wa siku zote, milele au ifananayo na milele.
Kibali hiki hutoka Kwa MUNGU mkuu, huyo ndiye mwenye kibali cha kudumu.
Kibali cha kudumu hutolewa na anayedumu milele. Ambaye hadumu hawezi kutoa kibali cha kudumu.
Mambo ya kuzingatia;
ππΎ Mungu hutoa vibali vya kudumu na vibali vya muda mfupi.
ππΎ miungu hutoa vibali vifananavyo na vyakudumu.
2. Vibali vya Muda visivyodumu.
Hivi ni vibali vinavyotolewa na miungu, watu au viumbe vingine.
ππΎ Majini, miungu, mizimu, na mashetani hutoa vibali vya Aina hizi.
ππΎ Wazazi hutoa vibali hivi
ππΎ Mke au mume hutoa vibali
ππΎ Baadhi ya viumbe kama wanyama hutoa vibali. Ndio maana Kama unafuga mnyama yoyote yakupasa umtendee wema maana kuna sehemu huchangia katika mizunguko yako. Watu wengi wanaowatendea wanyama mambo Mema hufanikiwa katika maisha yao.
Kibali ni Kama msingi/Password ya kufungulia njia Fulani uitakayo.
Katika maisha kila Jambo linahitaji kibali (maombi/password) ili lifunguke.
Yapo mambo ambayo mtu yeye pekeake anaweza jipa Kibali na likafunguka pasiposhida yoyote Ile. Lakini yapo mambo ambayo ynahitaji vibali kutoka Kwa wengine.
Watu wanapoenda ibadani huenda kuomba Vibali ili wafanikiwe katika Yale wayafanyayo, lakini sio kila kibali hutolewa msikitini au kanisani au sehemu yoyote ya ibada.
Vipo vibali vinavyotolewa na Mzazi, mke, mume, wanyama, miungu, Serikali, n.k.
Vibali vingi vina-expire hivyo ni muhimu kuvi-update ili kuvipa uhai. Vibali visivyodumu ndivyo vinahitaji kuvi-update.
Kwenye maisha wapo watu walioombewa vibali na wazazi au Mababu zao Enzi za kale, hivyo kwenye maisha ya sasa wao wanaona mambo yanaenda tuu kiurahisi mpaka ikafikia wakadhani ni jitihada zao ilhali sizo.
Biashara au Utajiri, ama mahusiano ya ndoa Kama unahitaji yadumu basi yakupasa uombe kibali cha kudumu kutoka Kwa MUNGU.
Lakini Kama unahitaji Utajiri au biashara au mahusiano yako ya ndoa yawe ya muda mfupi basi unaweza chukua kibali cha muda mfupi ambacho hupatikan Kwa watu Kama wazazi, wakwe, mke au mume, au mchungaji au Sheikhe au mganga wa kienyeji.
Katika kuomba Kibali kuna mambo Yafuatayo;
1. Kuomba Kibali kupitia umwagaji WA damu,
Hii ni Kwa wanaohitaji kibali kikubwa
2. Kuomba Kibali Kwa kupitia Utoaji wa Akili au utu wa mtu mwingine.
3. Kupata Kibali kupitia maji
4. Kuomba Kibali kupitia Moto
Hii hutumika zaidi katika vibali vya kiroho na shughuli zote za kiroho, na anga za mbali, Nyota za Mbali.
Kibali cha kutoa damu(Uhai WA Mtu mwingine) ni kibali cha kudumu na ndio kibali kikubwa Kama kikiombwa Kwa Mungu Kwa maana hata upande wa nguvu za Giza hutolewa pia.
Hakuna taifa lolote Duniani lenye nguvu ambalo limefanikiwa kwa Karne nyingi ambalo halijaomba kibali kikubwa cha kudumu kupitia Umwagaji wa damu wa watu wao wenyewe.
Wakati Mungu anataka kumpa Ibrahimu Kibali, alimtaka amtoe mwanaye Isaka Kafara. Lile lilikuwa tukio gumu lakini ililohitaji Jambo kubwa. Ili upate Jambo kubwa lazima ufanye Jambo gumu na kubwa. Ibrahimu alitakiwa kupewa kibali cha kuwa Baba WA mataifa.
Ingawaje Ibrahim hakumtoa Isaka Sadaka kimwili lakini kiroho tayari ilihesabika amemtoa Mwanaye Sadaka, dhamiri ya Ibrahim ilishakubali, alikuwa keshafanya uamuzi na tayari kiroho alishamtoa mwanaye Kafara.
Hivyo Yule Kondoo ilikuwa geresha au kivuli.
Sijui Kama naeleweka.
Sisemi watu wawatoe kafara watoto wao au ndugu zao, au wazazi wao, Hasha!
Nazungumzia Ili upate kibali sharti uwe tayari kuwapoteza au kumpoteza mtu muhimu kiroho au kimwili.
Kibali cha kudumu kinahitaji mtu mwenye uwezo wa kujitoa kafara kwa ajili ya wengine bila kujali maoni ya watu wengine.
Ili upate Jambo zuri yakupasa utoe Jambo zuri.
Ili upate Jambo kubwa yakupasa utoe Jambo kubwa.
Maisha yako yanahitaji KIBALI kikubwa ili kuyafanya yakutii wewe. Ukiogopa kuyapoteza maisha yako utayapoteza, lakini usipoyaogopa kamwe hautayapoteza, na hata ukiyapoteza basi utakuwa umeyaokoa maisha ya kizazi chako Kwa maana utakuwa umewaombea au kuwachukulia kibali kikubwa.
Kwa leo niishie hapa.
Ni Yule Mtibeli kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Mbezi Makabe, DAR es salaam