Kibamba - Dar: Maji Safi bado Changamoto, Wananchi watumia Maji ya Madimbwi na Visima

Kibamba - Dar: Maji Safi bado Changamoto, Wananchi watumia Maji ya Madimbwi na Visima

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Kwa Miaka 3 Wakazi wa Kata ya Mpigi Magoe, eneo la Torino-Kibamba wanadaiwa kutumia Maji ya Visima na Madimbwi ambayo si salama kwa Afya zao, licha ya eneo hilo kupimwa Miundombinu ya kupitisha Maji.

Mkazi wa eneo hilo, Irene Makea amesema kwa Miaka Mitatu wamekuwa wakijaza fomu lakini hawaletewi maji, amesema “Tumeambiwa tukifika watu 50 tutaletewa Maji, lakini hatujaletewa. Matokeo yake tunategemea kununua lita 20 kwa Tsh. 800”

Hata hivyo, Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( DAWASA) wa Kibamba, Elizabeth Sankere amesema bado wanashughulikia changamoto hizo kwa kuwa Miundombinu bado haijakamilika na kuna tanki la Msongamano linaloendelea kutengenezwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwaka jana alikuja waziri wa maji akiambatana na viongozi wa DAWASA na mbunge wa Jimbo la kibamba wakatuaminisha kuwa jimbo la Kibamba tatizo la maji limekwishwa lakini hadi Leo ni ndoto.

Mwaka umeisha hakuna cha maji wala dalili za maji. Mbunge wetu Mtenvu sijui yuko wapi.
 
Back
Top Bottom