Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Deus Kibamba, ameonya kuhusu kuongezeka kwa udhibiti wa vyombo vya habari na asasi za kiraia nchini, akisema hatua za kubana uhuru wa kujieleza na kuwazuia watu ni dalili ya mfumo unaotumia hofu kuficha mapungufu yake badala ya kuyatatua.
Akizungumza Juni 25 jijini Dodoma katika mkutano uliojadili utawala wa sheria, nafasi ya kiraia na marekebisho ya sheria nchini, Kibamba alisema hali hiyo inaashiria mazingira hatarishi ambapo hata mawakili wanaotetea haki za wananchi wanaanza kutazamwa kama maadui. Pia alieleza kuwa kuwepo kwa ishara za kuwazuia baadhi ya raia kusafiri nje ya nchi kunatokana na hofu isiyo na msingi.
Alisisitiza kuwa mamlaka zinapaswa kushughulikia changamoto zilizopo badala ya kutumia mbinu za kuwabana wananchi, akisema udhibiti wa kupindukia huashiria hofu ya kukabiliana na ukweli.
Aidha, Kibamba ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na vyombo vya habari kuendelea kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu haki za kikatiba, ili kuimarisha uelewa wa wananchi kabla nafasi ya uhuru wa kiraia haijazidi kupungua.