SoC02 Kibamia ya mtoto: Mama, baba au mlezi alaumiwe nani?

SoC02 Kibamia ya mtoto: Mama, baba au mlezi alaumiwe nani?

Stories of Change - 2022 Competition

Globomakaza

New Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Ikawa furaha kwa wazazi wote wawili kumpata mtoto wa kiume. Ikawa ni furaha zaidi kwa kuwa walimsubiri mtoto wa kiume kwa miaka mingi kwa hamu na shauku kubwa. Wakazipiga nderemo na vifijo kuuona uso wa mtoto wao wa kiume kwa mara ya kwanza. Maskini ya Mungu hawakujua ya kuwa kuna mengi yaliyoambatana na binadamu na ubinadamu wenyewe katika malezi ya mtoto wa kiume furaha iliyodumu kwa miaka mingi baadaye ilibadilika na kuwa huzuni katika maisha ya mtoto.

Kama ilivyokuwa kawaida kwa baba hata kabla ya kumpata mtoto wa kiume hakuwa mzoefu wa kukaa nyumbani, alipenda kusafiri na kuipiga miaka nenda rudi katika masafa ya mbali hasa akishampachika mkewe mimba alizoea kurudi mtoto akiwa tayari ni mkubwa. Kiufupi unaweza kusema kuwa baba alijua ya kuwa kazi yake ni kupachika mimba na hakutambua umuhimu wake yeye kama baba katika malezi ya mtoto. Hii haikuleta changamoto kwa watoto wa kike waliotangulia ila kwa huyo wa kiume.

Hapa baada ya baba kupachika mimba ambayo haikujulikana kuwa imebeba kiumbe wa aina gani,baba alichikichia na kwenda zake masafa ya mbali. Ilibaki ni kazi ya mama kulea mimba, kujifungua na hadi kulea mtoto. Ni hali ambayo kwa namna moja ama nyingine mama huyu alikua ashazoea. Angalifanya nini na wakati kile alichofunzwa ni kutii neno litokalo kwa mumewe? Mumewe hakuhitaji kuandika barua ya maombi ya kuwa nataka kusafiri bali ilitolewa kauli ambayo haikuhitaji kuhojiwa "nakwenda kutafuta"

Ikawa mtoto akiwa na umri yapata miaka saba,baba akiwa masafa ya mbali alipata taarifa kwamba kunako nyumbani alikwishapata mtoto wa kiume. Haikuhitaji kuzikata siku wala miezi bali safari ya kurudi nyumbani ilianza ghafla.Alipofika nyumbani ilikua furaha kwa wote baba kuliona toto lake la kiume lililojazana, toto afya inaita pia ilikuwa furaha kwa mtoto pia kumwona baba pia mama kumwona mumewe na mume kumwona mkewe ukweli baba alifurahia ujio wa mtoto wake wa kiume hapa duniani hadi akasahau suala la kusafiri kwenda masafa ya mbali.

Alipofikisha miaka nane tangu kuzaliwa kwake,mtoto akiwa darasa la kwanza alionekana kuwa na akili sana darasani akawa na uwezo mkubwa shuleni kitu ambacho kiliwafanya wazazi watamani kumsomesha mtoto ikawa hali ya kipato chao kiliwakatisha tamaa na kuona kuwa wao kama wao hawatakuwa na uwezo wa kumsomesha mtoto endapo ataendelea kufanya vizuri.

Kwa haraka baba aliwaza kumsafirisha mtoto kwenda kwa ndugu zake ambao walikuwa na uafadhali wa kipato. Kwa haraka aliwasiliana na ndugu zake waliokuwa wakiishi mikoa ya mbali ili mtoto akasomeshwe huko, na ndugu zake kwa upendo hawakusita walikubali ombi lake.

Upande wa mama haukuafiki wala kuridhia yaani mama hakukubaliana na wazo la mtoto yule mdogo kutengana na wazazi na kuelekea mikoa ya mbali hasa kwa kua kuna mambo mengi mazito aliyoyajua juu ya mtoto huyo.Lakini alikosa kuwa na kauli na maamuzi juu ya mtoto kwa maana jamii yenyewe ina desturi na utamaduni kwamba baba ndiye mwamuzi wa mwisho katika familia. Hivyo mtoto alipandishwa gari na kwenda zake mikoa ya mbali kujipatia haki yake ya elimu

Masikitiko makubwa ni kwa lile ambalo mama alilifahamu ila baba hakulitambua. Wakati mtoto anazaliwa (baba akiwa bado yupo masafa ya mbali), mama aligundua kua mtoto wake alikuwa na tatizo la afya ya uzazi. Wakati ule mama aliishi kupigana akitafuta dawa za asili huku na huku akiamini siku moja mambo yatakaa uzuri. Wakati baba amefika kutoka safari hakutambua yaliyojiri kwa kuwa hakuelezwa. Mbaya zaidi ni kwamba baba alikuwa akimwona mtoto akiwa na afya njema kwa macho kwa hiyo hakuwaza wala hakudadisi kuhusu afya ya mtoto.

Kiufupi ni kwamba maamuzi ya baba kumsafirisha mtoto kwenda mikoa ya mbali yalitenganisha huduma ya mama kwa mtoto na mbaya zaidi ni kwamba waliompokea kama walezi wapya wa kumsomesha mtoto hawakujua chochote

Akiwa ugenini mtoto aliishi miaka nenda rudi miaka mingi utoto ukimnyima kutambua kuwa yeye alikuwa na changamoto yenye uzito katika maisha yake. Aliishi kufurahia maisha ya kubukua na kufanya vizuri shuleni-akivuka madarasa na madarasa vidato na vidato hadi kufikia elimu ya viwango vya juu hapa sasa akawa ni mtu mzima. Wakati huu aligundua changamoto zilizombatana na maisha yake yaani alikuwa na kamdudu kadogo kenye kusimama kilegevu waswahili wanaita KIBAMIA

Hapa mtoto kama mtu mzima sasa alianza kutapatapa huku na huku akijaribu kutafuta dawa ya kumtibu mbaya zaidi aibu ilikua kubwa iliyomfanya ashindwe kuwashirikisha watu wenye upeo mkubwa.Matokeo yake ni kubugia na kunywa kila anachoambiwa na rafiki zake kuwa kitamsaidia-hata maji yakija kwenye chombo kichafu akaambiwa kuwa hii ni dawa aliamini kwa asilimia mia moja hivyo hata juhudi zake hazikua na mafanikio

Basi mtoto anaishia kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.
Hivi mie nilimkosea nini Mungu?
Wazazi wangu wangekukua nami wote mwanzo hadi mwisho ningelikua hivi?
Kwa nini mama alikubali niondoke wakati alijua kila kitu-ni woga kuwa angalipigwa na baba?au pengine hakua na elimu juu ya hili?
Kwanza mama alishindwa nini kumjuza baba au hata ndugu zangu walionipokea au ndo kukosa elimu au alihisi itakua aibu,asa si afadhali ungekuwa aibu ya wakati ule tu leo si mambo yangelikuwa gado
Ila baba na ndugu zangu kitu kimoja tu asa wanakaa na mtoto wasigundue shida alizonazo mtoto, dah?

Kiukweli utajiuliza maswali mengi lakini utabaki na jibu moja kwamba jamii ya leo inahitaji elimu kubwa juu ya hili suala linalopaswa kushughulikiwa utotoni mtoto anakuwa akiwa nalo hadi linakuwa sugu linakua zito kulitubu au linakua haliwezekani kabisa

Kama sehem ya jamii ni nini kinatakiwa kifanyike na kama ni elimu juu ya hili ikae katika mfumo gani ili jamii nzima ielimike, wazazi wakubushwe kuwakagua watoto wao na kugundua changamoto zao, elimu mashuleni-hii kwa vijana walio bize kubukua inakaaje.

Kwenu wapendwa limefika

MAISHA YA WATOTO WENU NIMEWAKUMBUSHA KUWA MNAWAJIBIKA
 
Upvote 1
Back
Top Bottom