Kibao cha Aziz Ally Mtoni na Historia Yake

Nikajua Aziz Ki Mzee wangu nisamehe bure. Lakini pia jitahidi utuletee historia ya mabingwa WA kihistoria Dar Young African. Asante baba
 
Nikajua Aziz Ki Mzee wangu nisamehe bure. Lakini pia jitahidi utuletee historia ya mabingwa WA kihistoria Dar Young African. Asante baba
The...
Niko mbali kidogo na mpira.
Sina la kusema nikafurahisha jukwaa hili.

Labda nijaribu kukumbuka yale niliyoyaona wakati wa utoto wangu kuhusu mpira:

YANGA NA SUNDERLAND UNAZI WA ZAMANI: KISA CHA MZEE MANGARA TABU NA AYUBU KIGURU

Nina rafiki yangu anaitwa Kazua leo asubuhi kanipa kisa cha Mzee Mangara Tabu na Ayubu Kiguru.

Wakati wa ujana wake Kazua alikuwa mkoba, yaani "centre half," wa Dundee United.

Leo mimi na sahib yangu Kazua akitutokea simba ghafla tumeliwa.
Miguu hainyanyuki ardhini haitaki inatukatalia sharti tuibembeleze.

Mzee Mangara Tabu alikuwa President wa Yanga na Ayubu Kiguru alikuwa shabiki mkubwa sana wa Sunderland na unaweza kusema ndiyo Haji Manara wa enzi hizo.

Haji mwanafunzi kwa Ayubu.
Ayubu alikuwa na kipaji cha ajabu.

Mtu wa vibweka lukuki.

Sunderland ikichukua kikombe asubuhi anakujanacho sokoni anakiweka mbele ya ubao wake washabiki wa Sunderland wakija sokoni wanatunza.

Hapo Ayubu kavaa jezi no. 6 ya Hamisi Kilomoni.

Jioni soko likifungwa anahesabu fedha zilizotunzwa anapeleka club Congo na Mchikichi.

Soko zima lile limejaa wanazi wa Yanga basi Ayubu peke yake anapambananao na mwisho wa siku wanasalimu amri wanafunga virago hao wanaondoka.

Ayubu alikuwa ana ubao wa biashara Kariakoo Market.
Siku hiyo Mzee Mangara kenda sokoni kununua mahitaji yake.

Ayubu kumuona Mzee Mangara akamuamkia kisha akamwambia, "Mzee Mangara kanunue hiliki tu basi. Vingine vyote vilivyobakia njoo uchukue kwangu bure."

Yanga ilikuwa imefungwa na Sunderland.
Mzee Mangara akamshukuru Ayubu kisha akamwambi, "Tutakutana Ilala Stadium."

Ayubu akamjazia vitu Mzee Mangara kwenye jumu lake, Mzee Mangara akimshukuru Ayubu akashika njia kwenda nyumbani kwake ambako hapakuwa mbali na sokoni.

Hapo chini soko la Kariakoo kama lilivyokuwa enzi hizo na Kazua ni huyo hapo picha ya mwisho.

NB: Kazua kafariki kiasi cha miezi mitatu iliyopita.
 
Mzee wetu wewe bahati baya upo bongo hapa ungekuwa nchi zinazojielewa huko kwa aina ya uandishi na maandiko ya kihistoria km haya ungekimbiliwa kama dhahabu.
 
Mzee wetu wewe bahati baya upo bongo hapa ungekuwa nchi zinazojielewa huko kwa aina ya uandishi na maandiko ya kihistoria km haya ungekimbiliwa kama dhahabu.
Covid...
Nimeandika na wao sana nikiwa hapa nyumbani.

Bahati mbaya mitandao imeua magazeti mengi yaliyokuwa yakichapwa London na kusambazwa huku kwetu.
 
Heshima kubwa Sana Kwako Baba yetu,Mzee wetu ndugu Mohamed said.
Wewe ni hazina kubwa kwetu Sisi vijana. Natamani kuwa kama wewe but my potentials are limited to poverty. Live long babaa
 
Sote ni masikini lakini huo umasikini ndiyo uwe kichocheo cha kutusukuma tusonge mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…