Kibarua cha Robertinho kipo hatarini

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Uongozi wa Simba Umeamua, Uongozi Wa Simba Umewasha Moto, Uongozi wa Simba This Time Around hawacheki na Mtu yeyote, Uongozi wa Simba This Time Ni Kimodaaa, Ni waya Ya Umeme.

Kwa Usajiri unaofanywa na simba hakika Sio Mapendekezo ya Kocha, Ni wao Kwa Utashi wao wameangalia Timu kwa Misimu Miwili ilikwama wapi wakaamua Kushusha Vifaa vya Kazi, Katika huu Usajiri Sidhani hata yule Scout Mpya aliye Tangazwa na Simba Kama Ameshiriki kuchagua hawa Wachezaji.

Makocha Mara Nyingi wachezaji wapya wanapo kuja kwenye timu huwa na Mapenzi yao kuliko uhalisia wa Viwango vya Mchezaji, Kocha Anaweza Kumpenda Mchezaji Na Kuona Kitu ambacho wengine wote hatuoni, Lakini Hawa Makocha Pia huwa na Eagle, Yaani Mchezaji Maarufu au aliye semwa sana katika usajiri wake Mara nyingi huamua kutokumtumia Kwa Makusudi Kabisa.

Kwa Upande wa Robertinho Wakati anafika Alimkuta Chama Akiimbwa sana Na Phiri Mechi yake ya kwanza Tuuu alimtoa Chama Kipindi Cha Kwanza, Bila Sababu za Msingi, Mpaka mashabiki walipo ingilia Kati tofauti na Hapo chama Benchi ndio lilikuwa Linamuitaaa, Same kwa Phiri Pamoja na Majeruhi lakini kuimbwa kwakwe sana Kumlifanya Robertinho Kumuweka Benchi Bila Sababu za Msingi hata wakati ambao hakuwa na Majeruhi, Hii Tabia Ipo Kwa Makocha Wengi Duniani……..

Sasa Usajiri wa Simba Msimu huu Umevaliwa Njuga na Viongozi waandamizi wa Simba, Na Wachezaji wote Usajiri wao Unaimbwaaa, Je Robertinho Anatafutiwa sababu ya Kufukuzwa? Leo Simba Tumetangaza Kumsajiri Luis M, Konde Boy, Ambaye ni Kipenzi cha wanasimba, Ni Kipenzi cha Rais Wa Heshima wa Simba na Tajiri namba 13 Barani Afrika Mo Dewji, Bila Kificho Boss anampenda Luis, Na Robertinho Kumuweka Benchi itakuwa ni Kujitafutia Lawama na Kuweka Kibarua Chake Mashakani.

Najaribu kuangalia namna ya upangaji kikosi wa Kocha wetu, Namna Anavyo Fanya Sub zake na Aina Ya Mpira anao Fundisha, Naangalia Usajiri wa Simba uliofanywa na aina Ya wachezaji walio sajiriwa naona Kama Ni Kama Robertinho Anakomolewa Kimakusudi na Viongozi wa Simba, Huenda Mechi Tano za Mwanzo ukijumlisha na Ngao ya Jamii, Zikaamua Hatma yake ya kuendelea kuwepo Simba au kutokuwepo. Huu ni Mtazamo wangu wa Awali, Simba Hawampangii Kikosi Kocha ila Kocha Anakaa kwenye Kikaango kama Itatokea Simba Kutokufanya vizuri Mechi 5 za Mwanzo huku akiwa na wachezaji Wenye Majina Makubwa Kiganjani mwake.

Fikiria Amuweke Benchi Akram kisa anataka Kibu Denis Acheze, Au Amuweke Benchi Onana Kisa Anataka Wazee wacheze, Au Ngoma Akae Benchi, Au Asimchezeshe Luis kama sio kutafuta kufukuzwa kazi. Nina wasiwasi na Robertinho huwenda Kikosi Ni kikubwa kuliko uwezo wake.


Muda utaongea Hadi September tutakuwa Tumejua Hatma ya Kocha wetu. Kila La Kheri Robertinho.
 
NATABIRI ROBERTINHO NDIO KOCHA ATAKAYEIMBWA KONA NA PEMBE ZOTE ZA NCHI HII 2023/2024
 
Ila Mpira Wa Tz Full Vitimbwi , Viongozi Wa Simba Na Yanga wanasajiri kiushabiki Zaidi kuliko mwalimu Anataka Nini Uwanjani

Hakika Angalia Sajiri Nyingi Utaona Kocha hakuhusishwa.

Sasa Atachagua Amuwekee Benchi Saido au Amuweke Benchi Usajiri Mpya
 
Ila Mpira Wa Tz Full Vitimbwi , Viongozi Wa Simba Na Yanga wanasajiri kiushabiki Zaidi kuliko mwalimu Anataka Nini Uwanjani
Walimu hawana maana. Anakwambia msajili huyu na yule, halafu yeye mwenyewe akipata ofa nzuri anaondoka na kuwaachia mizigo ya wachezaji wake. Kumbuka kocha Maki, akapendekeza aletewe Outarra na Okwa, baada ya wiki chache tu akapata ofa sijui Libya huko au wapi, akaondoka na kutuachia mizigo. Heri viongozi wasajili wenyewe maana ndio wenye timu. Kocha anaondoka muda wowote bila usajili, mchezaji aliyewaachia kuondoka hadi dirisha lifike
 
Pale real Madrid miaka yote usajili anafanya Perez na lazima acheze yaani umpe kocha uhuru wa kusajili mkubwa akiondoka kwani wachezaji anaondoka nao simba wamejifunza kwa zoran mak alivyomleta mchezaji wake mzungu pori simba wapo sahihihi kabisa.
 
Kuna watu mnaongelea mpira bila kuwa na uelewa wa mpira wenyewe.

Yani mchezaji awe mzuri uwanjani, alafu Kocha aamue kumuweka benchi kisa anaimbwa sana na mashabiki? Wakati performance ya wachezaji means timu ita perform vizuri, na hivyo Kocha atapewa sifa na KUKUZa CV YAKe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…