Kibarua cha siku 1 (Kesho - Jumatano)

Kibarua cha siku 1 (Kesho - Jumatano)

The bump

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,488
Reaction score
2,908
Kwa kijana anaetafuta kibarua cha kufanya apate hela ya kuishi kwa siku ya kesho anakaribishwa kujiunga nami.

Kibarua ni Kufyeka/Kusafisha/Kuchoma Moto Shamba la Heka Mbili.

Shamba Lipo Mlandizi, Usafiri Kuja na Kurudi ni Juu yangu.

Chakula: Asubuhi na Mchana ni Juu yangu.

Idadi ya wanaohitajika "WAWILI" Posho kwa kazi ni 10,000 per day.

Kwa muhitaji karibu PM,Tupange namna tunakutana POst hii ni ya Leo Date 22 aug 2023 itakua expired kufika Date 23 aug 2023

Kwa mtakaochelewa iona zingatieni hilo msije mkaja PM maana post haitokua na Kazi tena.

Mtu anae hitaji KULIMA akaribie Nagawa hili shamba kwa mkulima atakaehitaji ili aliweke safi muda wote alime mazao anayotaka.

Naweza Kukulipia KODI ya chumba nikakuwekea vitu vya kukaa ndani ili usimamie shamba tu, Mahtaji mengine Juu yako.

Muhitaji Karibu PM.
 
Acha unyonyaji, kusafisha shamba heka 2 watu wa 2 kwasiku uwape 10k? Navyofahamu heka inasafishwa kwa laki tena huko vjijini iweje hapo Mlandizi twn kabisa.
 
Acha unyonyaji,kusafisha shamba heka 2 watu wa 2 kwasiku uwape 10k?navyofahamu heka inasafishwa kwa laki tena huko vjijini iweje hapo mlandizi twn kabisa.
Very true...! Heka 1 ni laki huku mikoani.

Na inategemea na aina ya vichaka. Bei inaweza zidi kulingana na aina ya vichaka vilivyofungamana.....

Sharobaro kiepe yao..... KWA hiyo bei... Shamba litafyekwa mwezi.

Maana si unajifanya mchumi kulipa kwa day?

Hiyo ni kazi ya mauzo mkuu. Na unaweza pata mtu hukohuko....

Hata hivyo, hizo kazi zinafanywa na majirani.

Acha kujenga chuki na majirani! Unawanyima rizki
 
Mkuu shamba ekari moja kusafisha kwa elfu 10 ni sawa kweli?
Hauko peke yako na hata kama ungekua upo peke yako nadhani ndio maana limewekwa tangazo ili mtu aangalie anaweza au hawezi.
 
Kwa anae ONA anaweza TU anae ona ananyanyaswa. Atulie.

Haya ndio Maisha fanya unachoweza sio kwasababu kina LIPA. ila sababu una Kiweza.
 
Kama upo siliaz nakuhurumia sana ukimpata mtu akafanya iyo kazi kwa 10k niite mbwa na huyo mtu mm nitamwita mbwa nilichojifunza ww umenunua eneo hivi karibuni huna experience kabisa ya kilimo na program zake ndo maana unasema unagawa shamba mtu alilime bure
 
Back
Top Bottom