Mimi ni kijana niliyemaliza kidato cha sita(feb 2012) kwa mchepuo wa HGK, shule ya sekondari Galanos, mjini Tanga. Mahali nnapoishi kwa sasa ni Moshi mjini. Lengo la kushughulisha vidole na akili kwenye baobonya kwenye safu hii ni juu ya kiu ya kutaka kupata kazi ya hali yoyote kwa makubaliano. Hakika kazi ni muhimili wa maisha hasa kwa mimi kijana, Natumia nafasi hii kwa yeyote mwenye uweza au nafasi ya kunipatia kazi/kibarua ili ni kusogeza maisha na changamoto zake! UFANISI, JUHUDI NA NIDHAMU NI MUHIMILI YA MAENDELEO! Kwa ujuzi wa ziada nina ujuzi wa kiasi wa teknohama ya kompyuta na badhii ya 'programs' zake.