Kumezuka tetesi ya kujitoa kwa uwakilishi wa wakili Peter Kibatala katika kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani CHADEMA, ambapo taarifa hizo ziandai kuwa kuanzia wakati huo wakili Peter Kibatala alikuwa amejitoa rasmi katika kesi ya Freeman Mbowe.
- Tunachokijua
- Tetesi za kujiondoa kwa Wakili Peter Kibatala kwenye kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe zilianza kuzuka Novemba 10, 2021 kupitia Mtandao wa X (Zamani Twitter)
Mmojawapo ya watu waliotoa tetesi hizi ni Dr. Sisimizi aliyeandika ujumbe huu.
KIBATALA AJIONDOA RASMI KESI YA MBOWE
Jaji: Kama mnavyokumbuka Novemba 3, Kibatala aliwasiilisha ombi la kujiondoa kwenye kesi ya msingi, basi leo Karani ana majibu yake baada ya kushauriana na wazee wa Mahakama.
Mahakama imetulia iko tayari kusikiliza.
Jaji: Karani Ebu simama usome uamuzi wa Mahakama.
Karani: Mhe. Jaji kwa mashauriano na Baraza la Wazee, Mahakama yako Tukufu imeridhia maombi ya kujitoa kwa Wakili wa Utetezi Peter Kibatala.
Jaji: Sawa Karani sasa Kaa chini.
Tetesi hizi ziliwahi kuchapishwa pia kwenye mtandao wa YouTube mnamo Disemba 16, 2021.
Ukweli upoje?
JamiiForums imebaini kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli baada ya kuwasiliana na wakili Peter Kibatala.
Wakili Peter Kibatala aliendelea kumuwakilisha bwana Freeman Mbowe mpaka kesi hiyo ilipomalizika Machi 4, 2022 baada ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali kusema hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Freeman Mbowe alitiwa mbaroni akiwa Jijini Mwanza usiku wa kuamkia Julai 21, 2021 ambapo baada ya sintofahamu juu ya nani anamshikilia kiongozi huyu wa chama pinzani polisi walithibisha kwamba wanamshikilia na amepelekwa Dar es Salaam kujibu kesi iliyokuwa inamkabili pamoja na wenzake watatu wakituhumiwa kutenda makosa ya ugaidi na uhujumu uchumi.