Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,745
Kufuatia kuondolewa kwa jina la Rais wa TLS Tundu Lissu kutetea kiti chake TLS kwa kile kamati ya uchaguzi ilichodai aliyependekeza jina la Tundu Lissu ameshindwa kuthibitisha uhalisia wa fomu ya ugombea, kuna tetesi kwamba wakili msomi Peter Kibatala amepanga kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya kamati ya uchaguzi wa TLS mapema iwezekanavyo.
Kamati ya uchaguzi TLS imepitisha majina ya wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi TLS huku miongoni mwao akiwemo mwanasheria msomi machachari mwanamama Fatma Karume anayegombea urais akichuana na makamu wa Rais wa sasa Godwin Ngwilimi, wagombea wengine ni Godwin Mwapongo na Godfrey Wasonga. Katika nafasi ya makamu wa Rais kuna Rugemeleza Nshala.
Tarehe ya mwisho kukata rufaa ni tarehe 23 March 2018