Wala halina usomi. Ni uvunjaji wa katiba yetu ulio wazi. Wala haihitajiki Kibatala kumfanya mtu aelewe. Basi tu nchi inatawaliwa na washamba na wanaotawaliwa nao ni washamba. Bila katiba yenye checks and balances za kweli, haya mambo yataendelea sana.
Na ndio maana mafedhuli hayataki katiba mpya. Yanataka yaendelee kufanya ufedhuli bila kuzuiwa. Eti yanasema yanashughulikia maji, elimu na afya. Yalikuwa wapi kushughulikia hayo tangu 1961? Wanieleze ni nchi gani iliyoendelea ambayo siku moja ilifika hatua ya kuacha kushughulikia maji, elimu na afya? Haya ni mambo ambayo nchi zote zinaendelea kushughulikia mpaka mwisho wa dunia. Hata Marekani, UK, Japan... zinashughulikia haya mambo mpaka leo hii. Biden kasema bajeti yake kubwa inakwenda mwenye miundombinu.
Halafu yanasema katiba siyo sera yao. Akina JK, Waryoba, Butiku... ni UKAWA? Yaleyale aliyopita kukusanya maoni (Polepole, Kabudi, etc.) leo yanasema katiba mpya haihitajiki!! Yaani Tanzania hii ina watu mafara sana. Tena yanaongoza nchi eti! What a shame and disgrace to the country!!