Kibatala tena

Kibatala tena

Hapo sheria iko wapi, hiyo ni common sense tu, anapataga majinga. Kibatala wa kawaida tu namfahamu tangia anasoma Mzumbe, acheni sifa za kijinga
Duh!Kwa hiyo kuna uwezekano wewe unamfahamu Kibatala kuliko mama yake?Na hao wanaobanwa maswali na kushindwa kujibu ni mazuzu sana?
 
Aliyekuwa sheikh mkuu wa mkoa wa DSM ndg. Alhad Musa sasahivi ni mwekiti wa kamati ya maridhiano ya dini mvali mbali, inamaana Sheikh hajui kuwa dini ni moja tu?
Nani alikwambia Uislam hauna mahusiano na wengine?

Unaota?
 
Nani alikwambia Uislam hauna mahusiano na wengine?

Unaota?
Hakuna sehemu nimesema uislam hauna mahusiano na wengine bali nimetaka kujua kama uislam unatambua dini nyingine kuwa ni dini?
 
Hakuna sehemu nimesema uislam hauna mahusiano na wengine bali nimetaka kujua kama uislam unatambua dini nyingine kuwa ni dini?
Qur'an 3:83. Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa? 83
84. Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake. 84
85. Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri. 8586. Mwenyezi Mungu atawaongoaje watu walio kufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawafikia hoja zilizo wazi? Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu
 
Sehemu ya mahojiano ya Wakili Msomi Peter Kibatala na Mkuu wa upelelezi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, SSP Gerald Ngichi kuhusu kesi nambari 112 ya Mwaka 2018 iliyowahusu Freeman Mbowe na wenzake.

KIBATALA: Umesema Freeman Mbowe aliondolewa kwenye Mkutano na walinzi wake?

SSP Ngichi: Ndio

KIBATALA: Unawajua walinzi wa Mbowe?

SSP Ngichi: Siwafahamu.

KIBATALA: Sasa uliwezaje kuwatambua kuwa ni walinzi wake?

SSP Ngichi: Walikuwa wakimsaidia

KIBATALA: Kwahiyo kila anayemsaidia Mbowe ni mlinzi wake?

SSP Ngichi: Kimya.

KIBATALA: Mbowe alisema hatupaswi kuona kawaida wenzetu kunyongwa hadi kuuawa. Je unajua alikua anamaanisha nini?

SSP Ngichi: Hapana

KIBATALA: Kwahiyo Mbowe yupo sahihi?

SSP Ngichi: kimya

KIBATALA: Umesema Mbowe alisema kuwa haiwezekani wanaume wazima kama sisi tugeuzwe mandondocha. Je kuna tatizo gani kwenye maneno hayo?

SSP Ngichi: Huo ni uchochezi

KIBATALA: Wewe ni mwanaume au mwanamke?

SSP Ngichi: Mwanaume?

KIBATALA: Je uko tayari kugeuzwa ndondocha?

SSP Ngichi: Hapana

KIBATALA: Kwahiyo Mbowe yupo sahihi?

SSP Ngichi: Kimya

KIBATALA: Unadai Mbowe alisema Jacob Zuma alilazimishwa kujiuzulu. Je ni kweli au si kweli?

SSP Ngichi: Sifahamu

KIBATALA: Unadai Mbowe alisema Mugabe aling'olewa madarakani. Je ni kweli Mugabe aling'olewa au hakung'olewa?

SSP Ngichi: Sijui

KIBATALA: Unawezaje kufungua mashtaka kwa mambo ambayo hata wewe hujui?

SSP Ngichi: Sifuatilii vyombo vya habari.

KIBATALA: Unadai Mbowe alisema Rais Magufuli ni Mwepesi kama Karatasi?

SSP Ngichi: Ndio

KIBATALA: Maneno hayo yana shida gani?

SSP Ngichi: Magufuli sio mwepesi kama karatasi

KIBATALA: Wewe unaufahamu uzito wa Magufuli?

SSP Ngichi: Magufuli yupi?

KIBATALA: Magufuli aliyeandikwa kwenye hati ya Mashtaka

SSP Ngichi: Simjui

KIBATALA: Kwahiyo kwenye hati ya mashtaka mmeandika watu msiowafahamu?

SSP Ngichi: Aulizwe askari aliyeandika hiyo hati

KIBATALA: Kama wewe humfahamu kwanini unakataa kuwa si mwepesi kama karatasi?

SSP Ngichi: Kimya
Cross examination....
 
Hahaaaaa Kibatala ni smart sana, unapigwa maswali mpaka unajiona kalumekenge kabisa. Kimoyomoyo unatukana waliokutuma!!
 
Wataendelea kushindwa kujibu maswali kwa sababu hao polisi elimu zao za umande wanalazimishwa kufungua kesi ili kuwafurahisha wakubwa ambao kwenye hayo maswali ya wewe ni mwanamke au mwanaume wanakua hawapo..
 
Back
Top Bottom