Kibiblia mwanamke yoyote ukimkuta hana bikra huyo si mke wako

Revolution 22

Member
Joined
Jun 11, 2021
Posts
63
Reaction score
141
"Kibiblia mwanamke yeyote ukimkuta hana bikira huyo sio mke wako ni mke wa aliembikiri. Biblia inasema usimuache mke wa ujana wako ndoa ni agano na hakuna agano linafanyika bila damu. Agano la Mungu na wanadamu damu ya yesu ilimwagika.

Kwa hiyo agano la ndoa ni damu itoke yaani uone alama za ubikiri na mwanamke yule mwanaume wa kwanza aliembikiri huwa hamsahau kamwe" - Mchungaji Anthony Lusekelo(Mzee Wa Upako) akihojiwa Wasafi TV/FM
 
Kwani hatuambiani kila mara kwamba damu aliyoimwaga Yesu ndiyo ilikuwa ya mwisho na ikautakasa ulimwengu?Mbona tutachoka sana kwa vigezo na masharti ya kuzingatia maishani?
 
lusekelo mwenyewe mkewe hakumkuta bikra. kwahiyo hakuoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…