Kibo Complex ndiyo shopping center bora kuliko zote Dar es Salaam

Kibo Complex ndiyo shopping center bora kuliko zote Dar es Salaam

1. Mlimaji city complex
2. Quality center
3. Mkuki house
4. Msasani Mall
5. Kibo Complex
6. Masaki village
Hiyo Quality Center ni kama imekufa tu, nimeenda juzi nimeshangaa kwa kweli. Wafanyabiashara wengi wameondoka yamebaki mafrem na wachache wanaoendelea kukomaa. Sijui tatizo ni nini au ndo Magu kaharibu uchumi
 
Sasa kama hakuna umelileta kwa dhumuni gani humu mkuu???

Nilileta mada ili kupata maoni ya wadau wengine. Faida yake ni kuwa kuna malls na shopping centers zimetajwa hapa inabidi nifanye utaratibu nizitembelee nijionee kama kweli zinalingana na nilichokiona pale Kibo.
 
Hiyo Quality Center ni kama imekufa tu, nimeenda juzi nimeshangaa kwa kweli. Wafanyabiashara wengi wameondoka yamebaki mafrem na wachache wanaoendelea kukomaa. Sijui tatizo ni nini au ndo Magu kaharibu uchumi

Halafu kuna watu wanapalinganisha na Kibo!
 
Hahahhhh Hahahhhh, supermarket ya pale wamejaza t paper na chupa za maji, ina ubora gani
 
Nikiri kuwa sijatembelea shopping center nyingi ila kuna vigezo ambavyo nimevizingatia hadi kuja na tamko hili kuwa Kibo Complex ndiyo shopping center bora zaidi Dar es Salaam.
1. Utulivu - Ni sehemu ambayo haijazubaa lakini wakati huo haijachangamka kupita kiasi. Kwa watu kama mimi ni PERFECT kabisa.
2. Usafi. Kuanzia mazingira ya nje, ndani, vyooni, sehemu zote ni kusafi mno muda wote.
3. Usalama. Kwanza hakuna usumbufu wa walinzi ambao unaweza kukutana nao sehemu nyingi za aina hii. Hakuna mambo ya kuulizana unakwenda wapi, kusachiana. Unaingia kwa amani, unafanya shughuli zako unaondoka bila mtu yoyote kukubughudhi.
4. Huduma. Sina uhakika kama hii ni makusudi au imetokea tu kwa bahati. Wanajitajidi kuweka huduma zinazotofautiana. Hii inasaidia wapangaji wao kutokuwa na ushindani sana wao kwa wao lakini inatusaidia hata sisi kupata huduma nyingi zaidi.
Kuna shopping center gani mnaona inaweza kushindana na Kibo kwa vigezo hivi?
Ungemalizia " kwa mujibu wangu"
 
Hahahhhh Hahahhhh, supermarket ya pale wamejaza t paper na chupa za maji, ina ubora gani

Ila hapo hapo kuna maduka mengine unaweza kujipatia mahitaji yako ambayo umeyakosa kwenye hiyo supermarket. Kuna duka lile liko mlango wa kutokea nyuma unapata vitu fresh matunda, mboga nk.

Hawa jamaa inabidi wanilipe aisee!
 
Back
Top Bottom