Kiboko ya Wachawi alikosa connection ama connection ilipigwa ngeta?

Kiboko ya Wachawi alikosa connection ama connection ilipigwa ngeta?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Fredick Sumaye aliyekuwa waziri mkuu wa Mkapa aliwahi kusema. Ukitaka mambo yako yanyooke jiunge na CCM. Je, kiboko ya wachawi hakuzingatia huu ushauri?

Pamoja na sababu zote zitakazosemwa ku justify kifungo chake bado kuna wenzake waliotenda mabaya zaidi na bado wanadunda kwa raha zao.

Kuna kitu kisicho cha kawaida sana kwenye hili. Kifungo chake kimekuja baada ya kutokea tenguzi na teuzi.. Je ni coicedence tu ama kuna mambo yanalandana?

Unajua haya mambo ni connection, ni kushikana mikono, ni nipe nikupe. Viongozi wote wa kisiasa wana 'ma baba wao wa kiroho' ama viongozi wa kidini.

Hawa watu wamebeba siri nyingi sana za wanasiasa kwakuwa wameaminiwa na wao na wanawasaidia mambo yao mengi ya kiroho yaliyojaa ulozi na ushirikina mkubwa kwa kivuli cha dini.

Hawa viongozi wa kisiasa huwabeba na kuwalinda hawa wana dini kwa gharama kubwa mno lakini za kificho

Sasa hawa matapeli wa kidini huwa ni watembelea fursa na huwa hawawi na chanzo kimoja cha fursa. Fursa huleta sadaka nnono.

Fursa huwatambulisha sehemu muhimu.

Fursa huwapa nafasi ya kuheshimika na kutambulika. Fursa ni fursa, Fursa fursana!

Wajanja wanajua madhara ya kuwa na fursa chache. Kuna leo kuna kesho. Zikiondoka fursa mbali hakikisha unazo tatu kibindoni ili kujihakikishia ulinzi, connection na mapato.

Kiboko ya wachawi ana mengi ya kusimulia.. Tuupe muda wakata. Huu ni mwaka wa uchaguzi, vita vya wanasisa vinasambaa mpaka kwa.

20240728_191719.jpg
mafundi'
 
Alikataa kula na wakubwa, mwenzake wa pale Kawe anagawana sadaka na wakubwa.
 
Huyu ni kama zumarid wanakosa connection kwa kuamini nguvu zao pekee. Ukiwa kada hakuna kinachoshindana,sioni tofauti na hawa wengine walioachwa. Pili serikali haina kipimo cha kupima maudhui ya mtumishi.
 
Shida ilianzia baada ya utafiti wa mwananchi gazeti, sijui walilipwa na nani, hata hivyo ni heri mara dufu huo huduma kufungwa.
 
YULE ALIZIDI SANA HATA ANGEKUWA NA CONECTION WANGEMUONDOA TU

Jamaa alizidisha sana uhuni content za kuzalilisha watu matusi na utapeli hata angekuwa mwna ccm asingesavaivu

.Anasema chupi yako nikiiona naichungulia

.kuna siku kamtoa mtumishi mwenzie kasema mchawi kamfukuza
 
Wanadai Mwamposa kamkandia mwenzake
Mwamposa mzee wa kitengo .. Kawakamata wengi kama Wote.. Halafu top layers tupu😀
Huyu ni kama zumarid wanakosa connection kwa kuamini nguvu zao pekee.
Ukiwa kada hakuna kinachoshindana,sioni tofauti na hawa wengine walioachwa.
Pili serikali haina kipimo cha kupima maudhui ya mtumishi.
Wenzao wana backup
 
Wachawi wana nguvu sana ukiunuka kupambana nao ukiwashinda kiroho watakushinda kimwili kupitia mamlaka we si unaona kina kamchape lambalamba wakijitokeza tu hawamalizi mwezi lazima wazuiwe
 
Kiboko ya wachawi ni mgeni. Kwahiyo ameondolewa kwasababu atatangaza kwamba nchini kwetu kuna fursa za wajinga wengi na hii itaruhusu wageni wengi kuja nchini Kama manabii. Kwahiyo ni bora tunyonyane wenyew na wabongo wenzetu.
 
Kuna ndugu yangu alienda hapo akaambiwa amelogwa ndio maana kila akishika mimba zinatoka. Kiboko ya wachawi akamwambia ana majini watatu kila jini moja kulitoa ni million moja.

Yaani ili atolewe majini yote basi alipe 3 million. Hapo bado kumuona aliambiwa atoe 500k huyu ndugu yangu akalialia wakampunguzia hadi 200k ndio akamuona tapeli mkubwa yule.
 
Wachawi wana nguvu sana ukiunuka kupambana nao ukiwashinda kiroho watakushinda kimwili kupitia mamlaka we si unaona kina kamchape lambalamba wakijitokeza tu hawamalizi mwezi lazima wazuiwe
 
Kuna ndugu yangu alienda hapo akaambiwa amelogwa ndio maana kila akishika mimba zinatoka. Kiboko ya wachawi akamwambia ana majini watatu kila jini moja kulitoa ni million moja.

Yaani ili atolewe majini yote basi alipe 3 million. Hapo bado kumuona aliambiwa atoe 500k huyu ndugu yangu akalialia wakampunguzia hadi 200k ndio akamuona tapeli mkubwa yule.
Uoni kwamba ndugu yako ndo mwenye makosa
 
Back
Top Bottom