Kibonde afariki na mamilioni ya pesa za watu

Kibonde afariki na mamilioni ya pesa za watu

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,527
Reaction score
3,811
Poleni sana na msiba wa Kibonde.

Najaribu kuwaza, Kibonde ni MC wa masherehe mbali mbali. Kuna wakati tulitaka kumbook tukakuta imekuwa full booked kwa jumamosi za takribani miezi minne mbele.

Sasa najaribu kujiuliza, endapo marehemu alikuwa amepokea advance (kishika uchumba) kwaajili ya kuwa MC kwenye harusi za watu, je pesa hizo ndugu zake watarudisha? Waliolipa kwa Mpesa Tigo Pesa au bank atleast wapo salama. Je, vipi kwa waliolipa cash? Yani walionana na marehemu kisha wakalipa na hawakuandikishiana popote pale

Kwa uhodari na jina alilokuwa nalo Kibonde kwenye ushehereshaji basi yawezekana kabisa kuwa atakuwa amefariki na pesa nyingi za watu waliotoa advance.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hapo watanzania tujifunze kusaini kwenye makaratasi hata pesa kidogo tunayolipa au kupokea. Makubaliano yanayohusu pesa bila kusaini mkataba iko siku utakula hasara.
 
Maisha ni zaidi ya pesa!
Binadamu mwenzako amepoteza uhai, watoto wake, familia yake, wafanyakazi na marafiki wanamlilia, hata kuzikwa bado hajazikwa, wewe unachowaza ni uwezekano wa pesa za sherehe alizochukua kwamba zitapotea! Tujifunze kuwa na angalau chembe cha ubinadamu
 
Maisha ni zaidi ya pesa!
Binadamu mwenzako amepoteza uhai, watoto wake, familia yake, wafanyakazi na marafiki wanamlilia, hata kuzikwa bado hajazikwa, wewe unachowaza ni uwezekano wa pesa za sherehe alizochukua kwamba zitapotea! Tujifunze kuwa na angalau chembe cha ubinadamu
Pesa haina ndungu wala hisia...
 
Si busara sana kuongelea hili lakini lina maana sana.

Kwa kipindi hichi na maisha jinsi yalivyo ni ngumu kuweza kuziba pengo la pesa iliyokwisha pokelewa. Mathalani Kibonde alikuwa ni MC mkubwa na expensive. Ghalama yake si chini ya miliioni na nusu. Sasa kama amelipwa advance ya laki nane au hata million na alitakiwa kuifanyia kazi juma mosi hii, je kutakuwa na uwezo wa ku replace hiyo pesa!!!! Maana MCs wanapatika na wataziba pengo la uwepo wa Kibonde, je hiyo pesa itapaikana as soon as possible? Maana MCs wakimaliza shughuli anahtaji umkamilishie pesa yake on the spot.

Hata kama familia itahtaji kulipa madeni, it will be too late. So kwa kiasi flani hili jambo litaleta changamoto lakini hamna namna,

Any way, mi bado narudia kusema

"mwili ukikataa pesa haina nafasi" apumzike mahala pema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BABA TUPAC leo umeongea jambo la muhimu mno, niliwahi kumuuliza mchungaji mmoja kuhusu hii sheria ambayo inatumika na waislamu baada ya kifo waislamu sharia ni kuwa hakuna kuzika mpaka marehemu asafishwe madeni yake yote, ndio maana kabla ya kumsalia inatangazwa `waumini sasa tunaenda kumsalia ndugu yetu na kumuombea dua, lakini kabla ya hapo kama kuna mtu yoyote anamdai marehemu aje hapa amalizane na ndugu zake` siku moja pale ilala msikitini alijitokeza jamaa anamdai marehemu milioni 30 ikawa kimbembe. Jirani yangu mchungaji aliniambia hata kwao pia ipo hio ila sema huwa inamezwa na uombolezaji na hakuna anaekumbushia. Kama ndugu wa kibonge ama msiba mwengine wowote mlipieni marehemu madeni yake au mkubali kuyabeba kwenye shingo zenu ili ndugu aende kwa bwana akiwa msafi.
 
Back
Top Bottom