Kibonde ashangazwa na wanafunzi kufeli, adai enzi zake alikuwa moto wa kuotea mbali

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi ambaye ukimpa topic hawezi kukosa cha kuchangia, jana alishangwaza na baadhi ya wanafunzi kufeli mitihani yao huku wengine wakichora makatuni kwenye mitihani yao ya mwisho. Kibonde alidai enzi zake anasoma Azania alikuwa ana uwezo wa kupata A masomo yote na anakumbuka B alipata mara mbili pekee.

Anadai juhudi zake katika masomo zilimfanya akapata shule nzuri ya Ilboru ambapo aliendeleza moto ule ule kabla ya kufaulu na uko pia vizuri ambapo aliamua kutokwenda chuo na kuamua kufanya kazi katika kampuni moja iliyompa ofa nzuri ya kazi.

Pia amewaomba sana wadogo zake wanaomsikiliza washikilie elimu ili waje wapate mafanikio kama aliyonayo yeye ambapo baada ya nasaha hizo lilikuja tangazo la biashara.

Jamani mliofanikiwa kusoma naye ndugu Kibonde ebu tukumbusheni ni jinsi gani huyu jamaa alikuwa mahiri enzi zake.
 
OK HATA KAMA JAMAA HAKUWA KIPANGA DARASANI, KWA SASA NI KIPANGA KWENYE MAISHA.. Mafanikio yake ni makubwa sana kimaisha na wengi wameshindwa.. kama hivi 1. Ni mtu maarufu sana tanzania popote anaweza kupata msaada 2. Yupo kwenye media kubwa tanzania anakutana na fursa nyingi. 3. Amefanya matangazo mengi ya company kubwa tanzania hizo company zilijua ni mkali ndio zikamchukua 4. Ni balozi na mtoa taarifa wa mashirika ya nyumba tanzania huko ndio kunampa mapesa mengi kuanzia posho, mshahara na kujengewa.. etc kifupi jamaa ni akili kubwa katika maisha japa darasani sifahamu.. maisha si darasani bali ni mtaani na huyu jamaa ameibuka THE CHAMPION
 
kwani kuna mtu kasema hakuwa kipanga
 
Hakuna anayesemaga yeye alikuwa mkia shuleni cha msingi awasihii tu watoto wapende kusoma na sio sifa za kijinga
 
Na kama kweli alichaguliwa Ilboru "enzi hizo" si suala la kubahatisha kuwa alikuwa kipanga.
 
Hayo maelezo yako yalitakiwa yaje kama NB.
Majibu ya msingi kwa swali lililoulizwa bado haujayatoa. Wewe umeanza na kusema kwamba "hata kama jamaa hakuwa kipanga", kwani kuna mtu kasema hakuwa kipanga?
 
kwani kuna mtu kasema hakuwa kipanga
UANDISHI WAKO UMEKAA "KIDUMANZI" Kama ulijua alikua na uhakika alikua kipanga ungetoa direct message.. nadhani hata wewe ulikua hujua kwamba jamaa ni mtu mwenye mafanikia makubwa maishani ndio nimekujuza hayo mafanikio niliyotoa hapo juu ni makubwa kumuita THE CHAMPION
 
Nimekumbuka hili: KILA BABA ANAJIGAMBA ALIKUWA MKALI WA HESABU ENZI ZAKE hahahahahahaha
 
Jamani uongo mwingine watu wafikirie kwanza kabla ya kusema.
 
Hayo maelezo yako yalitakiwa yaje kama NB.
Majibu ya msingi kwa swali lililoulizwa bado haujayatoa. Wewe umeanza na kusema kwamba "hata kama jamaa hakuwa kipanga", kwani kuna mtu kasema hakuwa kipanga?
HUO UANDISHI UNAELEKEA HUKO KWENYE KUJARIBU KUPINGA JAMAA SIO KIPANGA KUNA THREAD PIA NIMEIONA ... KIFUPI JAMAA YUPO VIZURI SANA...
 
Nimekumbuka nyumbani..
Hasa wale wadudu wanaobiringisha udongo...


Kibondeeeeeeeee
 
Hata kama hakuwa kipanga kasema ukweli mtupu watoto wa leo sijui akili zao zinatumika kufanya nini
 
Hiki ni kichekesho! Hongera profesa Kibonde... Bahati mbaya tamaa ya pesa ilikatisha ndoto zako za kupaa kielimu...
 
Hata mi cwezi sema kwa wanangu kuwa nlikuwa ki.LA.zzzaa darasan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…