Kibu arudisha pesa za kwenye account ya Simba

Kapata dharula,(changamoto) akiwa likizo ameamua kurudisha pesa ili watafute mchezaji mwingine kabla ya dirisha kufungwa, je kafanya vibaya?
Mkataba alosaini na simba unasemaje kuhusu dharula
 
Mkuu Scars ebu tupe ufafanuzi hapa,kibu ndio kishavunja mkataba hapa bado,maana ndio yale yale feisal uliedai exit clause ni kurudisha pesa tu
Inategemea na Mkataba unavyoeleza, kama makubaliano yaliandikwa kuwa upande utaovunja mkataba utalazimika kurudisha pesa za signing fee kisha atakuwa huru basi Kibu atakuwa ametekeleza matakwa ya mkataba.

Ila navyojua Simba haiwezi kuweka kipengele chepesi kama hicho, kwasababu thamani ya kuvunja mkataba haitegemeani na thamani ya mchezaji aliyosajiliwa nayo.

Mchezaji anaweza kuwa amesajiliwa hata kwa milion tano lakini kwenye kipengele cha kuvunja mkataba bila sababu ikawekwa bilion 2.
 
Simba walimuingizia mpunga akiwa zake Marekani. Kama kumshawishi abakie Ili akirudi tu aje adondoshe wino. Kwa ujumla kulikuwa na makubariano ya mdomo tu. Hivi sasa kunzia leo ndio Simba wameshtuka wako mbioni kuhangaikia namna ya kufoji mkataba na sahihi ya kibu
 
Swali fikirishi kwakuwa simba wanauzoefu wa kuvunja mikataba na makocha kirahisi sana hivi mikataba yao ikoje, tumeshuhudia wengine wakienda kuuguza Kwa kufunga wenyewe vilago, walio wengi kufungiwa vilago, (pack and go)
 
Hela za Mkataba zinarudi bila makubaliano mengine tena..hawa jamaa nani anawadanganya kufanya hivi kama kweli atakua karudisha hela bila kukaa mezani kafanya mambo ya kiboya sana..
Hawa simba wapuuzi walishupalia fei kurudisha hela tena badi hamed ally alikuwa anashabia sasa hivi jasho linamtoka
 
taarifa ya kwanza sweeden ya pili norway kama hamna uhakika mngesema yuko ulaya mapumzikoni
 
Tsh ngoea tuwaone nyie wazungu,ila nilikuambia Trend itakuwa kama ya Fei.Inaitwa Fei style.....
Walishaambiwa wakati wa sakata la Fei kuwa tunaweka precedency mbaya hawakusikia. Leo ipo kwao wamruhusu aendelee na mambo yake kwa kuwa amesharudisha fedha na kulipa mshahara wa mwezi mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…