- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kibu Denis Kaiomba radhi Simba SC kupitia akaunti yake ya X, amesema mtoto akinyea mkono haukatwi.
- Tunachokijua
- Mdau wa JamiiCheck alitaka kujua uhalisia wa andiko linaloonekana kuwa ni la mchezaji wa Simba SC Kibu Denis lenye ujumbe wenye ishara ya kuomba msamaha kwa Klabu yake kufuatia sakata linaloendelea kati yake na Klabu yake
Mnamo, tarehe 23 Julai 2024 klabu ya Simba SC ilitoa taarifa rasmi ya Kibu Denis Prosper kutoripoti Kambini nchini Misri ambapo timu hiyo ilikuwa inafanya maandaalizi ya msimu mpya 2024/2025.
Baada ya sakata hilo umesambaa ujumbe ambao unaonesha kuandikwa na Kibu Denis ukionesha ujumbe wa kuomba radhi, ujumbe huo unasomea: " Maisha yana safari defu katika utafutaji, mtoto akiunyea mkono haukatwi".
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa andiko hilo la mtandao wa X sio halisi, bali limetengenezwa kwa kutumia jina la mchezaji huyo.
Aidha, JamiiCheck imefuatilia ukurasa rasmi wa Instagram wa Kibu ambao bio yake inaeleza bayana kuwa hana akaunti katika mtandao wa X wala FaceBook na katika ukurasa huo hakuna taarifa yoyote inayohusiana na ujumbe huo wala ujumbe wa kuomba radhi ulioandikwa kwa namna nyingine haupo.
Jamiicheck imejiridhisha kuwa ujumbe huo ni wa kuzusha na chapisho hilo si la Kibu Denis bali limehaririwa kwa kuwekwa jina la mchezaji huyo na kuongeza alama mbele inayoonesha tick ya buluu ili kujaribu kuhadaa kwa kuonesha ni ukurasa uliothibitishwa.