Kibu ana vibes la kutafuta goli, yumkini hana maarifa ya kufunga magoli, hana maarifa ya kiifundi kushawishi walinzi lakini ana nguvu na muandaaji wa pirika pirika za kutafuta magoli.
Walimu wanajua kazi na umuhimu wake akiwa kiwanjani, ila mashabiki na watazamaji huwa hatuna muda wa kumjaribu na kumstahamilia mchezajibwa aina yake.
Binafsi sipendi namna anavyocheza, huwa namuona kama kituko uwanjani. Uchezaji ule unasababishwa na uwezo wa maarifa yake kichwani naamini wachezaji wa namna yake huwa hawawezi kucheza kiushindani ulaya, wanafeli mchana kweupe kwasababu ya kiwango kidogo cha uchakataji mawazo uwanjani.
Muangalie MAYELE, aziz key, Chama, yule mwamba wa DRC aliye tufunga juzi tuu Taifa hapo.
Usiniambie sitoi mifano ya watz, wapo ila majina nimesahau. Kwa mfano Fei, angekuwa mtulivu zaidi kiwanjani angeweza kucheza mchezo wa kuvutia zaidi.
Wachezaji wetu wingi hawana football intelligence kasoro ambayo inachangiwa na kiwango kidogo cha elimu ya darasani.
Unasema nini? Kwamba elimu ya darasani haina mahusiano na akili ya mpira kiwanjani? Elimu ya darasani inakuza kiwango cha general intelligence ya mchezaji wa mchezo wowote. Ndio kigezo cha mwanzo kinachochangia emotional intelligence ya mtu. Hivyo ikiwa ndogo hiyo usitarajie kupata wachezaji wenye uwezo mzuri.
Muangalie Aziz key, Evar Meza wa Azam FC hawa jamaa ukiwaona tuu unajua mwisho wa maisha yao ya mpira watakuwa walimu.
Alaa mziki
Nakubali kukosolewa na kubadilika