PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Bila ya kujalisha upo timu gani, bila kujali ni wakina nani waliopo nyuma ya Kibu Denis, wapenda soka wote wanapaswa kumlaani kwa alichowafanyia Simba.
Simba wamemtoa Kibu huko walipomtoa, wakampambania katika changamoto alizozipitia, wakampa nafasi lakini hakuwapa chochote cha maana zaidi ya kuifunga Yanga, Simba wakasimama naye, wakamuimba na akaimbika.
Striker, aliyeimbwa na kutegemewa na akapewa kila mechi lakini mwisho akaumaliza msimu kwa kuifungia Simba goli moja tu, lakini bado Simba waliendelea kumuamini, wakamuimba, wakawa tayari kumrekebishia maslahi yake, lakini akawaanzishia vituko vya kipumbavu kabisa na mwishowe akawatoroka.
Mpira wa Tanzania unazidi kukua na kupewa heshima, kadili unavyokua inapaswa wachezaji wajifunze sana kuhusu elimu ya mikataba, pia wajitambue kuwa wao ni wadau muhimu sana na upumbavu wao unaligharimu soka la Tanzania pakubwa na huenda ikapelekea lirudi likikokuwa.
Simba inafahamika kwa jinsi ilivyo na ushirikiano pale wachezaji wake wanapopata malisho mapya nje, huwa haiwang’ang’anii. Kuna wakati Simba huonekana kama Soca Academy badala ya Professional footbal club sababu tu wakati wowote wachezaji wake wakionekana huko nje huwa ipo tayari kuhatarisha mipango yake na kuruhusu wachezaji kuondoka.
Angekuwa ni Chama amewafanyia haya ningemuelewa, lakini siyo Kibu Denis.
Soma=> Kibu kuisumbua Simba, Taswira mbaya kwa timu