Kibu Denis

No.2 itoe ile siyo assist ni rebound.
 
WEWE NI TOPOLO TENA LILO ZEEKA.

Yani wewe unaakili kumzidi Pablo aliyefundisha Real Madrid.

Pablo kamwani Kibu, Paulsen kamwamini Kibu, wewe kajamba nani unakuja kubwabwaja humu.

Hivi unaweza hata kupiga danadana!?
Hoja yako ni ya kijinga na ya kimazoea sana. Wewe ndio wale wanaoamini mtu hupaswi kukosoa mchezaji Kwa sababu anafundishwa na mtu mwenye taaluma ya ufundishaji mpira!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu hafai kbs nilimuona na Ruvu hakuna mtu kbs
 
Siku Kibu akicheza mpira wa maana na kufunga magoli utasema ana papara tena?
 
Sasa mbona unasema kuna kitu ambacho wewe na Mimi hatujaona mbona umetujumuisha sisi ktk mtizamo wako wewe binafsi??umetujumuisha bila kutuomba.Wewe kama unaona hivyo unavyoona jitaje mwenyewe usijumuishe na wengine.Andika upya bandiko lako
 
Tumpe muda wa kukomaa. Akipunguza papara akawa na utulivu wa Chama...atatupa goli nyingi sana huyu
 
Huyu jamaa sina hakika kama anaweza kupiga hata danadana
 
Uko sahihi .
Nilichogundua watanzania wengi wanashabikia mpira hawajui mpira na hawaamini kwenye utaalam .

Tunapaswa kujua yafuatayo :-
1 . Mchezaji yeyote anapikuwa mpya kwenye timu anapaswa kupewa muda kuzoea mazingira na mfumo wa timu aliyohamia . Kibu ana kipaji cha soka na anajua mpira . Sema hizi timu za Kariakoo huwa zinanataka mchezaji afike tu na kuanza kufanya maajabu . Kuna uhusiano kati ya muda na ufanisi . Tumpe muda Denis .

2 . Tunapaswa kuwapa nafasi makocha wanaomuamini . Hakuna kocha atampanga mchezaji mwenye kiwango kibovu wakati ana wachezaji wengine wazuri .
Makocha wa Simba na Taifa stars siyo mbumbumbu kama baadhi ya mashabiki wa soka wa bongo .

3 . Uwanjani kuna mambo mengi mbali na kufunga tu . Unaweza kufunga magoli halafu ukashindwa kuyalinda . Uwanjani kuna kukaba nafasi , kukaba mtu , kumiliki mpira na kutoa pasi . Inawezekana Kibu haya anayafanya vizuri na kusaidia timu kuliko kufunga .

Mimi naamini ktk kumpa muda mchezaji mgeni ktk nchi , timu au mfumo mpya .
Pia tusisahau pia mtu anaweza kuwa na changamoto nyingine nje ya uwanja zinazomuathiri mchezaji .
Tuwaachie wataalam wa timu washughulike na wachezaji , sisi tulipe viingilio na kushangilia timu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…