Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Simba sasa hiv inabebwa sana na Kibu Dennis, huyu mwanaume amefika hapa kwa sababu ya zomea zomea yetu mashabiki wa Simba kwake, alikuwa akifanya makosa mengi sana kiasi kwamba tulidhani hastahili kuchezea Simba, nayakumbuka sana maneno ya Mzee Magori alipomzungumzia mchezaji huyo wakati akiongea na Mahmoud Zubeiry katika kipindi cha azam sports , alisema huyu Kibbu ni mchezaji mkubwa sana, uchezaji aliokuwa nao kule Mbeya City utakuwa tofauti na Simba, kweli leo nayaona, Kibbu ana stamina ya kutosha, ana kasi ya kutosha, uwezo binafsi wa kutosha, ana control ya kutosha, ana mashuti ya kutosha, nini kitamfanya Kibbu asicheze soka ulaya.
Namtabiria makubwa sana mwanaume huyu wa shoos, leo kule Singida amenyimwa goli dhahiri kabisa, ameruka hewani kuliko hata kipa Metacha mwenyewe, ndio maana juzi niliomba sana viongozi wa Simba Kibbu arudi sana nchini kwa ajili ya mechi hiyo muhimu leo.
Ubaya Ubwelaaaa