Kiburi cha Kinyonga

Kiburi cha Kinyonga

zegamba180

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
820
Reaction score
541
Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, mbwa, Paka na Kinyonga walikuwa wameenda kwa mfalme kumsalimia. Sasa wanyama wengine wakawa wanaomba zawadi toka kwa mfalme kasoro kinyonga.
Kinyonga akawa anazungusha macho mbele nyuma juu chini. Wenzake wakapewa zawadi nyingi.
Jion wakamwaaga mfalme tayar kwa kuondoka.

Ng'ombe: Kinyonga mwenzetu mbona hukuomba zawadi?

Kinyonga: kwa jinsi nilivyokuwa namtazama mfalme asingeweza kunipa.

Mbuzi: kwanni kinyonga?

Kinyonga: kwani hakuona kama mimi nilikuwa nahitaji zawadi? Si aliona ni mimi pekee sikuomba.
 
Hii story ina ujumbe mzuri sana. Maana yangu ni hii;
Kuna baadhi yetu tunapoenda kanisani ama msikitini hatumwelezi MUNGU mahitaji yetu, tukiamini anayajua na anajukumu la kututatulia. Kinyonga kazi kuzungusha macho, ndivyo baadhi yetu tufanyavyo. Kitu ambacho sio sahihi. Tunapaswa kusema hitaji letu kwa MUNGU.
 
Back
Top Bottom