Maujohnsimba
JF-Expert Member
- May 20, 2018
- 246
- 225
Habarini wandugu.. Kuna ndugu yangu anasumbuliwa sana na kichefu chefu na kutapika na kinaanza asubuh tu akiamka akisha jisaidia hajakubwa mambo yanaharibika.. Amepima vipimo vingi vya damu hakuna kinachoonekana amefanya endoscopy majibu mazuri amefanya abdomen ct scan kilakitu kipo sawa.. Mwezi wa nane huu anatapika kila siku asubuh.. Msaada mwenye kujua tafadhali.