Kicheko wa Efm achukuliwa Clouds

Unapofanya mahojiano na chombo chochote cha habari jitahidi uchague cha kuongea na si lazima ujibu kila unachoulizwa vingine ni binafsi na vinafaa kubaki binafsi kwakuwa maisha bado yapo na mwisho wa siku utabaki wewe kama wewe (usijiharibie)
Unapofanya mahojiano kama hayo epuka kabisa kumponda mwajiri wako wa zamani kwakuwa hakuna mkamilifu na huyajui ya kesho
 
Kweli kabisa kaka
 
Siku hizi wachekeshaji na wasanii ndio wanapata kazi za utangazaji wale waliosomea kazi wanayo
Mpoki,Giggy Money,Idris,Bi Hindu,Swebe,Kicheko,Monalisa,Zembwela,Feza Kessy
 
Watoto wa kishua bhana... eti EFM ndio wameanzisha Singeli!! Huku Ushenzini tupo na Singeli miaka na miaka sasa halafu mtu aseme EFM ndo wameianzisha!!! Ni kama mtu aseme Radio One ndio walianzisha Charanga hata kama ishakufa kibudu!!!!

Mkuu hata Ziwa Tanganyika wanasema aliyelivumbua ni mzungu, David Livingstone kama sijakosea.

Wakati wabongo tulikuwa tunaliona kabla hata huyo mzungu hajazaliwa.
 
kama kuna maslai anayoona yatamtoa mwache asaini shavu coz hayo ni maisha yake mi namtakia kila la kheri
 
Mkuu hata Ziwa Tanganyika wanasema aliyelivumbua ni mzungu, David Livingstone kama sijakosea.

Wakati wabongo tulikuwa tunaliona kabla hata huyo mzungu hajazaliwa.
Sawa Mkuu lakini pamoja na yote hayo, hao Wazungu waliishia kusema "tumevumbua!" na sio "tumelianzisha!"
 
Sawa Mkuu lakini pamoja na yote hayo, hao Wazungu waliishia kusema "tumevumbua!" na sio "tumelianzisha!"

Kwa hiyo hao jamaa inabidi wawe wanasema EFM imevumbua Singeli.

Nimekusoma mkuu.
 
Huko kapotea kabisa na walioziba nafasi yake Efm wanafanya poa zaidi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…