Juzi nimeambiwa habari za kushtusha na inabidi nizitoe kwa serikali yetu. Inasemekana kuna Mtanzania ambaye anakaa Kenya mpakani na Tanzania kwa upande huu wa Mkoa wa Mara. Huyu Mzee kazi yake kubwa ni kununua Dhahabu za kimagendo ambazo hazilipiwa kodi. Inasemekana hiki ndicho kichochoro kikubwa cha kupitisha dhahabu kutoka Tanzania halafu wanatafuta njia Kenya ya kuzipeleka Dubai.
Kibaya watu wanajisifia kwamba huu ni mpaka ambao wanahonga kidogo tu na kupita na tayari wana watu wao pale mpakani. Vitu kama hivi ndiyo vinafanya kuwe na kodi za ajabu kwansababu wafanyabiashara/wachimbaji wadogo wadogo wamekuwa vinara wa kukwepa kodi. Tanzania ikipata kodi kwa njia za madini na nyingine ambazo kwa sasa watu wanachenga itapunguza maumivu makubwa ya kodi nyingine kwa masikini.
Watanzania tuweombe risiti na kuhimiza hivi vitu vya kimachinga vilipiwe kodi. Lakini tukiona mabaya tusisubiri na kujiona kama vile hayatuhusu maana mwisho wake yanatuhusu.