Kichomi kwa kiingereza kinaitwaje?

Kichomi kwa kiingereza kinaitwaje?

inategemea kinachoma wapi huwezi kiita abdominal pain wakati kinachoma mgongoni utakuwa unatulisha matango poli
 
Tunahitaji Kamusi ya Kitabibu kwa kweli. ...

Kuna kisa nilisumiliwa, New Parents wamempeleka mtoto kwa Dr alikuwa anasumbuliwa na Kwi Kwi...sasa hawakujua jina lake kwa kingereza. ...

Dr anauliza mtoto anashida gani mzazi anasema kwikwi /quick quick....

Ilichukua mda mpaka yule mtoto alipata tena KwiKwi wakiwa pale kwa Dr..ndio ikabidi wamuonyeshe Dr.

Yule mtoto aliishia kupewa jina la Hiccups....kama utani....na amekua nalo watu wa nyumbani wanamwita hivyo.
 
Hii imenikumbisha nikiwa primary kweli mtihani waliuliza taja magonjwa 3 yanayotibika kwa njia ya chanjo nikasema kichomi kwa maana navyoelewa kichom ni kama kuna damu kuganda kwa hyo unapiga chale kidgo kwa wembe basi panapona
 
Mzuqa

Nimeshikwa na kichomi hapa mzigoni yani kimenikalisha. Msaada kwa kiingereza kinaitwaje?

Nimecheki kwenye google translate eti cinnamon wakati cinammon ni ile aina ya spices. Google walifanya makosa kuwapa wakenya tender ya kutranslate kiswahili yan. Ndio hawahawa wanakuja na majina mapya ya kiswahili mabaya na ya ajabu mfano password eti nywila WTF!

Msaada kichomi kwa kiingereza

Sky Eclat
Kitu chenye ncha kali
 
Back
Top Bottom