Kichwa cha mbuni mchangani

Kichwa cha mbuni mchangani

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Imezungumzwa sana na wahenga kuwa mbuni anatumbukiza kichwa mchangani kujificha wakati mwili mkubwa unaonekana nje. Ni aina fulani ya kujidanganya.

Tanzania kuna mahali tumefikia tumekuwa kama mbuni! Chama kikongwe cha CCM kuna mahali kimefikia kujifanya kama mbuni!!
Nimeisikiiza hotuba ya Rais huko UN na kwa kweli lafudhi na matamshi ya kiingereza yalinikosha sana lakini nahisi kuna mahali tumegeuka mbuni hasa katika UVIKO na demokrasia.

Baada ya mlipuko wa UVIKO 19 dunia yote inajua hatua kama nchi ambazo tulizichukua na matokeo yake (ya faida na hasara) lakini leo tunazungumza kivingine kama sio siye.

Kuhusu demokrasia,wote tunajua wazi kuwa 2020 uchaguzi ulichafuka mno kwa dhahiri kabisa na badala ya kutuambia "vibrant democracy) tungekausha tu ili tuje turekebishane huku nyumbani.

Demokrasia hiyo hiyo leo hii kuna wenye haki ya kufanya watakalo na kuna ambao hata kuvaa fulana yenye maandishi "Tunataka katiba Mpya" ni kosa la kusababisha kuzungukwa na mitutu.

CCM wanatamba na ushindi wa kishindo lakini ndani ya dhamira zao wanasutwa na yaliyofanyika, HILA na UJANJA utatubeba kwa muda gani na mwisho wake utakuwa nini?

Tuyakubali matatizo yetu,tuyaweke mezani na tutafute namna ya kwenda mbele.
 
Kwa hiyo nchi ina watawala wenye tabia na hulka kama za mbuni!! Yaani kila sehemu ni umbuni umbuni tu.
 
Mbuni hajawahi kuficha kichwa mchangani kwa nia ya kujificha, ni binadamu huwa tunapenda kusambaziana taarifa wasizozielewa za kimbea.

Sourse:
download (4).jpeg
 
Back
Top Bottom