Kichwa cha mtoto kuwa na joto kali wakati sehemu zingine za mwili kuwa kawaida

Kichwa cha mtoto kuwa na joto kali wakati sehemu zingine za mwili kuwa kawaida

KASRI

Member
Joined
May 2, 2009
Posts
93
Reaction score
22
Wasalaam JF,

Nina mtoto wa miezi saba (7) ambaye tangu akiwa na miezi minne amekuwa na tabia ya kuwa na joto kali kichwani wakati sehemu zingine za mwili zipo na joto la kawaida. Hii imekuwa ikitokea mara kadhaa hasa usiku. Nilimwona Dr wa watoto nikamweleza akasema inawezekana ni VIRAL infection kwa hiyo itakwisha yenyewe. Sasa anamiezi saba na hiyo hali imekuwa ikijirudia.

Naomba ushauri kwa anayefahamu au aliyewahi kukutana na hali kama hii

Natanguliza shukurani
 
mkuu kimbia hospital fasta umuone doctor atakusaidia. Mia
 
Huyo dokta uliyemweleza tatizo la mtoto akakujibu litaisha lenyewe ni dokta wa kuungaunga NENDA HOSPITALI KUBWA ONANA NA MADAKTAR BINGWA WAMCHUNGUZE MTOTO KWA UNDANI NA UMAKINI WATAGUNDUA TATIZO NA WATAMTIBU, mtoto anateseka ni vile hawezi kuongea
 
Uko wapi nikuelekeze?Je tatizo ni kichwa kupata moto tu au ana shida nyingine?Anakula vizuri,anakua/ongezeka uzito nk,maana wakati mwingine tunahisi joto letu na si la mtoto labda kama utakuwa n a themometa upime joto wakati anamoto,vinginevyo ni hali ya kawaida kwa watoto
 
huyo lazima awe mwana siasa au mwana sayansi maneke anafikiria sana kuleta maendeleo nchi hii
 
Wasalaam JF,

Nina mtoto wa miezi saba (7) ambaye tangu akiwa na miezi minne amekuwa na tabia ya kuwa na joto kali kichwani wakati sehemu zingine za mwili zipo na joto la kawaida. Hii imekuwa ikitokea mara kadhaa hasa usiku. Nilimwona Dr wa watoto nikamweleza akasema inawezekana ni VIRAL infection kwa hiyo itakwisha yenyewe. Sasa anamiezi saba na hiyo hali imekuwa ikijirudia.

Naomba ushauri kwa anayefahamu au aliyewahi kukutana na hali kama hii

Natanguliza shukurani
Mambo vip kaka hii inshu yako uliisolve maana mwanangu anashida hii pia
 
Wangu wa kwanza nilikuwa namshangaa ila nikagundua kuwa Luna meno yalikuwa yanaota..
Huyu wa pili wala sijaumiza kichwa.
Nahisi ni meno pia yanawasumbua watoto wenu.(
 
Wangu wa kwanza nilikuwa namshangaa ila nikagundua kuwa Luna meno yalikuwa yanaota..
Huyu wa pili wala sijaumiza kichwa.
Nahisi ni meno pia yanawasumbua watoto wenu.(
Mkuu hayo meno yalikua ya juu au ya chin? Wa kwangu ameota ya chin lakin cha moto ikifika mida ya jioni
 
Mkuu hayo meno yalikua ya juu au ya chin? Wa kwangu ameota ya chin lakin cha moto ikifika mida ya jioni
Yote mkuu yalikuwa yanafanya kichwa kinakuwa cha moto kabisa l. Ila sikumpeleka hospital japo aklikuwa anaendesha si haba. Nyonyo kwa sana.
 
Yote mkuu yalikuwa yanafanya kichwa kinakuwa cha moto kabisa l. Ila sikumpeleka hospital japo aklikuwa anaendesha si haba. Nyonyo kwa sana.
Nimekusoma mkuu mimi kaendesha kwelikweli kamaliza wiki iliyoisha ila kwa sasa amestop alikua anapewa nyonyo kwa sana na maji kwa wingi. Ila kwa sasa naona kichwa ikifika mida ya jioni kinakua cha moto....
 
Back
Top Bottom