Kichwa cha Tumbusi na maajabu yake

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
10,677
Reaction score
11,768
Habari mabibi na mabwana, bila shaka ni wazima, na mida hii kila mmoja wetu yupo kwenye mihangaiko yake ya kujitafutia mkate wa kila siku.

Nisiwachoshe sana twendeni kwenye dhumuni la habari hii.

Habar hii naileta kwenu kama story, lakini ni story ya kweli wala sio alfulela ulela.

Ushawahi sikia habari za kichwa cha tumbusi (huyu tumbusi ni ndege) na maajabu yake?

Kama ushasikia basi Unaruhusiwa kuongezea nyama, kama bado ngoja nikumegee kidogo.

Kuna mzee wangu mmoja huyo anaishi Wilaya ya Balama, kata ya Mavala, kijiji cha Sapamueto, ndani ya mkoa wa Cabo del Gado.

Huyu mzee ni mjumbe wangu wa kamati ya ufundi (mganga wangu).

Kwa muda mrefu sana huyu mzee nimekua nafanya nae kazi (issue zangu nyingi huwa namshirikisha) na mara nyingi kazi zangu zinaenda kama ninavyo taka.
...........................................
...........................................
ANGALIZO : Mimi ni mchimbaji, na madini bila ushirikina utakua unasindikiza watu tu.
***************

Kikawaida nikimuona mganga ni mtaalam kweli (sio tapeli) hupenda kumuomba anifanyie vitu ambavyo sintaweza kumsahau mganga huyo.

Kwanza napenda kumuomba anisafishe mwili wangu (kunipa kinga ya mwili wangu dhidi ya husda za wachawi)

Siku moja nilienda kumpa shukrani mzee wangu (hapa kuna issue ilienda kama nilivyo taka) baada ya maengezi ya hapa na pale, nikamgusia kuusiana maswala ya kinga ya mwili wangu dhidi ya uchawi.

Mzee akazama ndani ya makablasha yake na kunitolea kichwa cha ndege.

Akaniuliza unamjua TUMBUSI?
Nikasema sijawahi kumuona lakini hilo jina sio geni masikioni kwangu.

Akatoa kile kichwa na kunikabidhi nikiangalie.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::

Nakuja mida si mirefu.
 
Haya bhana, tuwekee kabisa na namba za huyo mzee wa Gado, ili Pm zipungue ikiwezekana na kapicha kabisa ka huyo mzee maana bila hivyo, tangazo halitanoga!
Usisahau kuweka na bei za huduma yake!
 
Kuna mdau aliniita kidogo akanipe Ramani za kazi, si unajua kazi zetu bila intero huchelewi kujikuta uko nyuma ya nondo.
::::::::::::::::::::::::

Nilikiangalia kile kichwaa, kinavyo onekana ni chamda mrefu sana.
Mzee akaniuliza ushawahi sikia watu wanafanya mabalaa lakini kuwakamata inakua tabu?

Akaniambia, siri imejificha hapa sasa.
Akaniambia huyu ndege hupenda kuruka juu sana lakini akitua jua lazima eneo hilo litakua na mzoga.

Kiufupi huyu ndio bingwa wa kuotea.

Akaniambia ni kikuchanjia huyu we utakua na machale kama yeye mwenyewe Tumbusi.

Sikutaka nijiulize sana, nikamuomba anichanjie.
Kwakua ilikua ni mida ya jioni akaniomba tungoje ifike kesho, maana kuna mizizi mingine inahitajika kuchanganywa.

Asubuhi na mapema mzee alitoka kuelekea zake mstuni, mpaka mida ya saa 4 mzee alikua tayari kesha rudi na madawa kibao.
Nilisubiri mpaka mida ya jioni ndipo mzee akaniita uwani mwa nyumba yake nakutoa kikopo kidogo chenye mchanganyiko wa madawa yaliyo pondwa nakua vumbi.

Alinipa ndoo ya maji yenye majani ndani yake nakuniamuru nikaoge.
...........

Kuna jambo na malizana nalo kwanza, nakuja mida hii hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…