Kichwa kuuma kupita kiasi tatizo kubwa ni lip?

MankaM

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
9,448
Reaction score
3,065
Habarini za asubuhi wapendwa wa JF natumaini mu wazima.

Nahitaji msaada wenu juu ya hili tatizo nini kinasababisha kichwa kuuma sana hata ungetumia dawa tatizo liko palepale inafika kipindi unaboreka sana na kukosa amani.

Msaada tafadhali.
 
Pima BP ndugu yangu, la sivyo stroke inaweza kuwa mojawapo ya tatizo linalokuja.
 
Kichwsa cha depression (msongo wa mawazo huwa akisikii dawa) km kuna jambo hat km ni moja tu na linasumbua sana akili yako jaribu kulibeba km lilivyo na usiliweke sn moyoni kiasi cha kukuumiza kchwa na utafute ufumbuzi wake km inawezekana km haiwezekani achana nalo angalia mambo mengine... mimi nina ushuhuda wa hili, niliugua kichwa kwa muda wa mieze kma nane nahangaika hosp sipati tatizo.. nilikutana na doctor mmoja pale TMJ na alinisaidia sana kugundua tatizo... haikuwa ugonjwa bali depression... alinidadisi mambo mengi na kunisii niwe wazi... niliongea nae kwa kirefu sana na alinipa ushauri ambao mpk sasa namshukuru mno mno. so jaribu kuangalia na ww inawezekana kuna kitu kinakusumbua... kichwa cha depression hakisikii dawa
 

asante mkuu na mimi nimepata kitu hapa.
 
Kuna sababu nyingi za kuumwa kichwa!
Hata sijui nianzie wapi kutoa ushauri!
Ngoja kwanza niwapishe wachangiaji wengine!
 
Kuna sababu nyingi za kuumwa kichwa!
Hata sijui nianzie wapi kutoa ushauri!
Ngoja kwanza niwapishe wachangiaji wengine!
Kuwa na Malaria,matatizo ya macho,kukaa muda mrefu bila kupata usingizi,kukaa juani muda mrefu,matatizo ya pressure,matatizo ya moyo,mawazo mengi,endeleeni jamani........jamani jamaa anahitaji msaada wa haraka.
 
Ukiona kichwa kinauma au maumivu yeyote mwilini ambayo hayajasababishwa na ajali au jeraha, basi ni ishara kuwa mwili wako unazidiwa na asidi, kiasi cha alkaline kimepunguwa sana huku asidi inazidi kujijenga.


Maji huzuia na kuponya kabisa maumivu mbalimbali mwilini:

Ishara za mwanzo kabisa za asidi kuunguzwa ndani katikati ya seli au kwa maneno mengine asidi kuzidi kwenye seli za mwili na madhara ya kijenetiki ambayo yanaweza kujionesha, ni maumivu mbalimbali yanayozidi kujitokeza katika mwili.
Kutegemea na kiasi cha upungufu wa maji mwilini na namna na eneo lenyewe asidi ilipojijenga (ambayo ingeondolewa kwa kuongeza kunywa maji tu), maumivu maalumu ya mwili hujitokeza!

Maumivu hayo yanajumuisha; kiungulia (heart burn), maumivu ya moyo (angina), maumivu sehemu ya chini ya mgongo (lower back pain), yabisi (rheumatoid), maumivu ya kichwa (migraine headaches), homa za asubuhi kwa kina mama wajawazito na maumivu mengine mengi unaweza kuyataja.

Watu wengi siku hizi hawawezi kuishi bila kumeza aina fulani ya dawa ya kupunguza maumivu.
Ni rahisi kuelewa namna gani maumivu ambayo hayajasababishwa na ajari au maumbukizo yanavyoweza kujitokeza mwilini.

‘Namna hii rahisi ya namna maumivu yanavyotengenezwa mwilini imetupumbaza wengi wetu sisi katika taaluma ya madawa tangu binadamu alipoanza kutafuta suluhu ya maumivu ya mwili kwa kutumia dawa – dr Batmanghelidj'.

Viwanda vya madawa vinatumia mabilioni ya fedha kutafiti dawa hizi na zile za kuondoa maumivu na mabilioni mengine zaidi hutumika kutangaza aina fulani ya dawa za kuondoa maumivu.

Upungufu wa maji mwilini (dehydration) unaweza kutibiwa kwa kuongeza kunywa maji tena bure bila gharama yeyote.
Ili kuuelewa mfumo wa utengenezwaji wa maumivu mwilini, tunahitaji kwanza kujifunza namna usawa wa asidi na alkalini unavyofanya kazi mwilini.

Hali ya uasidi husababisha kuunguzwa kwa baadhi ya miishio ya neva mwilini. Kunapotokea hayo, ubongo huonywa juu ya mabadiliko hayo ya kikemekali ya kimaeneo, ambayo sote hutafusiri kama MAUMIVU. Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea sisi kusikia maumivu.

Kwa kawaida wakati damu yenye maji ya kutosha inapoizunguka seli, baadhi ya maji huingia ndani ya seli na kutoa nje molekuli za haidrojeni. Maji huisafisha asidi toka ndani ya seli na kuiacha sehemu ya ndani ya seli katika hali ya ualikalini ambayo ni hali yake ya kawaida na ya mhimu.

Kwa afya bora kabisa, mwili unatakiwa kubaki katika hali ya 7.4 katika kipimo cha ph (potential hydrogen).
Hali hii huhamasisha afya kwa sababu ndiyo hali inayoviwezesha vimeng'enya vinavyofanya kazi ndani ya seli ambavyo hupata ufanisi mzuri katika ph hii. Utiririkaji wa kutosha wa maji ndani na nje ya seli huifanya sehemu ya ndani ya seli kubaki na kuhimili hali yake ya kiafya ya kiualikalini.

Ndani ya miili yetu, figo husafisha haidrojeni iliyozidi ambayo husababisha asidi toka katika damu na kuiweka katika mkojo unaozarishwa. Kadiri mkojo unavyozarishwa kwa wingi ndivyo mwili unavyojiweka katika hali ya ualikalini kirahisi zaidi. Hii ndiyo sababu mkojo unaokaribia rangi ya uweupe ni kiashiria cha kufanikiwa kwa mfumo wa uondoaji wa asidi mwilini, wakati mkojo wa rangi ya njano au chungwa ni ishara ya kuunguzwa kwa asidi mwilini.

Watu wanaodhani kwenda uani kwa ajili ya haja ndogo mara mbili au tatu kwa siku ni usumbufu kwao na hivyo kuacha kunywa maji ili kuzuia hilo hawana uelewa wa namna wanavyohatarisha miili yao.

Ubongo unalindwa vizuri zaidi dhidi ya asidi kutokana na ukweli kuwa unapata umhimu wa kwanza katika kusambaziwa maji kwa ajili ya mahitaji yake yote. Sehemu zingine za mwili haziwezi kuwa na bahati hii wakati maji yanapokuwa yanapatikana kwa njia ya mgawo. Ingawa upungufu wa maji unapobaki kwa muda mrefu, ubongo pia huathiriwa kutokana na hali ya uasidi katika seli, hivyo hali kama za kupoteza kumbukumbu na magonjwa ya mishipa hujitokeza.

Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa kuwa alkalini.

Kwa kunywa glasi moja (ml 250) ya maji halisi na kuchukua kipande cha chumvi ya baharini, kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa maumivu.

Jaribu hii kwa kunywa glasi moja ya maji na kisha kuiweka chumvi mwishoni mwa ulimi wako na kuiacha iyeyuke kwa dakika na kisha isafishe kwenda chini na glasi ya pili ya maji. Kwa mjibu wa dr.Batman, kitendo hiki kitabadili PH ya damu, tishu, ogani na seli ndani ya mwili.


KAMA SULUHU YA HARAKA: KWA MUDA WA SIKU 2 KULA MATUNDA TU (usile chakula kingine) NA JUISI YA MATUNDA ULIYOTENGENEZA MWENYEWE GLASI 2 KILA BAADA YA MASAA 2 NA NUSU, unaweza pia kutengeneza supu ya mbogamboga na ukala. Baada ya siku 2 utajisikia nafuu sana na unaweza kunipa feedback unaendeleaje.

http://maajabuyamaji.net/maumivu-3/
 
Kuwa na Malaria,matatizo ya macho,kukaa muda mrefu bila kupata usingizi,kukaa juani muda mrefu,matatizo ya pressure,matatizo ya moyo,mawazo mengi,endeleeni jamani........jamani jamaa anahitaji msaada wa haraka.
Typhoid, vidonda vya tumbo, mafua, upungufu wa damu, depression, baadhi ya dawa na dawa za kulevya(mfano bangi, kuvuta petroli, dawa za kutibu malaria, dawa za kuongeza nguvu za kiume), kuangalia sana computer kwa karibu, kusoma muda mrefu huku umelala chali, masturbation, jamani endeleeni kutaja.......................
 
pole kwa tatizo si ajabu unamatatizo kama ya ugonjwa wa yphoid, vidonda vya tumbo, upungufu wa damu, depression, baadhi ya dawa na dawa za kulevya, , kuangalia sana computer kwa karibu, msongo wa mawazo na mengine.
jitahidi kuuchunguza mda wako hasa matumizi ya simu kwa mda mrefu na komputa au kusikiliza mziki kwa sauti ya juu sana
MWISHO
JITAHIDI
- kufanya mazoezi kila siku
- kunywa maji ya kutosha
- tumia virutubisho vya kuosha mwili( kutoa sumu mwilini) km tianshi lipid management tea na mashine kama kitana cha tiens chenye uwezo kukusaidia kwa tatizo lako kiitwacho ACU COMB twaweza wasiliana kwa ruhazwentaki@gmail.com, ruhazwentaki@yahoo.com au +255755569494
 

nafarijika sna kwa msaada kama huu itabid niufanyie kaz ila kwa ishu ya mawazo.........
Eee mola niepushie jaman
 

nashukuru mkuu kweli kuhusu maji najitahid sana afu na matunda sana tu kuhusu mawazo sina ila nina mambo mengi yananizonga kichwan na siwez yaepuka kadri siku zinavozid ndo yanaongezeka kama kupungua ni kwa uchache sana nahis ndo yanayoongeza tatizo ntajitahid kwa hilo
 

kwa pc sawa na kusoma mda mrefu bt hapo kwe upungufu wa damu umenitisha sana mkuu
 

nahis hiko kichwa ndo kinanisumbua
 

somo zur sana hili mkuu wangu ulikuwa wapi siku zote hizo??
 
Angalia wingi wadamu itakuta una damu nyingi,kumywa maji mengi damu iwe nyepesi kusafirishwa,punguza mawazo
 
kwa pc sawa na kusoma mda mrefu bt hapo kwe upungufu wa damu umenitisha sana mkuu
Ni kweli, ukiwa na upungufu mkubwa wa damu, oxygen perfusion kwenye brain inapungua.unapata dull aching headache(yaani kuna maumivu ya kichwa ya mara kwa mara, uchovu, kushindwa kufikiri vizuri[poor concentration]) na dalili zingine nyingi).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…