Kidato cha 4 kuanza mtihani Novemba 11, 2024, Idadi ya watahiniwa yapungua ukilinganisha na mwaka 2023

Kidato cha 4 kuanza mtihani Novemba 11, 2024, Idadi ya watahiniwa yapungua ukilinganisha na mwaka 2023

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Idadi ya watahiniwa wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2024 kuanzia kesho Novemba 11, 2024 imepungua kutoka 572, 338 mwaka 2023 hadi kufikia 557, 731 mwaka huu.

Akitoa taarifa ya maandalizi ya mtihani huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohamed amesema katika idadi hiyo wavulana ni 250, 562 na wasichana ni 278, 759.

Amesema maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika kwa Tanzania Bara na Zanzibar, katika vituo vyote ambavyo ni pamoja na shule za sekondari 5, 585 na 961 kwa watahiniwa wa kujitegemea.

Kadhalika NECTA imeonya kuchukua hatua kali za kisheria kwa wanafunzi pamoja na shule zitazobainika kuwa na viashria vya udanganyifu.

Soma pia:Wanafunzi 572,338 kuanza Mtihani wa Kidato cha 4 leo

 
Kila lakheri kwa watahiniwa wote wa kidato cha nne.

Mungu awajazi maarifa, afya njema na kujiamini katika kipindi hiki cha mitihani.
 
Back
Top Bottom