Kidato cha sita 2013 wanatakiwa kuripoti JKT 24/06/2013

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
TANGAZO


MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-

1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.

2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.

3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.

5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.

6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.

===================================

Selections hizi hapa:
Endepo tovuti ya JKT itakuwa ngumu kufunguka, angalia hizi attachments from JF

===================================

Kwa maelezo zaidi ya kambi mbali mbali walikopangwa angalia Jeshi la Kujenga Taifa
 

Attachments

Ha ha ha ha.. Kuna watu hawaendi hata kwa fimbo... Mtoto wa marian, feza boys, marygoreth, st marys, shaaban robert etc umpeleke JKT.. Hii ni zaidi ya siasa

Kuna watoto kibao wako busy na big brother the chase majumbani kwao na wengine wameanza short course na tempo kwenye kampuni za baba zao uwaambie wakasote JKT.. Nani atakubali?
 
Mkuu akhsante kwa taarifa.

Vp kuhusu watoto wa kiislam!
Maadili yao yatazingatiwa, ama ndo ule ule mfumo kristo kuhakikisha kuwa unawekwa utaratibu wa kuwavua hijabu zao.
Kama mwanafunzi hataki nini effect yake?
 
Mbona tangazo linasema wanatakiwa ku-report mach 2013.
 
Mkuu akhsante kwa taarifa.

Vp kuhusu watoto wa kiislam!
Maadili yao yatazingatiwa, ama ndo ule ule mfumo kristo kuhakikisha kuwa unawekwa utaratibu wa kuwavua hijabu zao.
Kama mwanafunzi hataki nini effect yake?

Mumeanza mambo yenu! Jeshi halina dini mkuu huko ni mwendo wa bukta na green vest tuu.
 
mwanamke wa kiislam ambaye alikuwa science na alikuwa ana div. 1,
atatakiwa avae hijab yake? Ama hijab haitakiwi?
 

Sasa siku hizi kuna PRIVATE SCHOOLS na Wanaochagua BRITISH or AMERICAN SYSTEM of EDUCATION na ni WaTANZANIA halafu; Wanaingia CHUO KIKUU ina Maana kwasababu waliotumia AMERICAN SYSTEM hakuna hizo DIVISION --- wanaweza kukwepa bila JKT MATATIZO?

Sasa, Wengine wanaopata DIV IV au 0; Ina Maana hawahitaji kusota kwenda JKT? Unajua ENZI ZILE kuna watu walikuwa wanapata DIV I 'O' LEVEL lakini 'A' LEVEL anafeli lakini haina maana ni Wajinga... sasa hivi ni Ma-ENGINEER...

Kwahiyo hapo JKT inabagua???
 
Ngono za kulazishwa kwa watoto wa kike,hata wa sasa wanalalamika,ni majanga mapu,wavulana hamna neno mana kule hakuna uliberali.
GIRLS AT DANGER,NOT PROTECTE TO THOSE WHO FORCE SEX TO THESE GIRLS.
 
Mbona ubaguzi sasa whta about division III and IV..!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…