KIDON, unawajua hawa? The deadliest killing machine

KIDON, unawajua hawa? The deadliest killing machine

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,555
Reaction score
6,972
KIDON ni kitengo ndani ya Mossad chenye jukumu la kufanya mauaji dhidi ya wale wenye kuhatarisha usalama wa Israel. KIDON ndio wanaosifika na kuogopwa zaidi duniani katika kufanya assasinations kwa ufanisi na ufasaha wa hali juu


Neno Kidon ni la kiyunani lenye maana ya ncha ya upanga, hili lina akisi jinsi kitengo hiko kilivyo mahiri na hatari katika kufanya mauaji.



Kidon ilianzishwa miaka ya 70 kutoka katika kitengo cha Caesaren kilichokuwa chini ya Mossad kufuatia kuuawa kwa waisrael 11 waliokuwa washiriki katika mashindano ya Olympic mjini Munich Ujerumani mwaka 1972. Mauaji hayo yalifanywa na wapiganaji wa kipalestina, japo waisrael wengi walikufa wakati polisi wa Ujerumani walivyojaribu kuwaokoa mateka. Na mara moja baada ya kuundwa wakapewa kazi ya kuua kila aliyehusikia na mauaji hayo ya waisreal kazi iliyofanyika kwa mafanikio makubwa japokuwa kuna wahanga nao walikufa

Mbali ya kuwa kitengo hiki kuwa chini ya Mossad lakini kutokana na usiri wake mkubwa hakina ofisi ndani ya makao makuu ya Mossad mjini Tel Aviv. hata ma-agent wake ni vigumu kutia mguu makao makuu, hii ni kwa mujibu wa afisa wa zamani wa intelijensia katika kitengo cha Mossad kinachoratibu shughuli za Kidon bwana Mishka Ben-David katika kitabu chake "Duet in Beirut". Anaendelea kusema kuwa hata majina wanayotumia ni majina ya kufikirika na si majina rasmi, na wakiwa shughulini hutumia jina la 3 la mhusika na mara nyingine hadi utambulisho wa 4 na wa 5. kutoka na usiri na ufanisi wa hali ya juu, kitengo hiki kimepachikwa jina la Mossad ndani ya Mossad

Recruitment katika kitengo hichi ni kutoka katika special forces wenye vipaji vya hali ya juu ndani ya
Israel Defence Force (IDF) na hupatiwa mafunzo ya hatari kwa mda wa miaka 2. hawa jamaa wanasifika kwa kutoacha alama yeyote katika assasinations zao na wamekuwa wakifanikiwa kwa miaka mingi

Wauaji hutumia pasi na nyaraka feki za mataifa mbalimbali za kusafiria zilizofojiwa kwa ustadi wa hali ya juu na wataalamu wao au hutumia pasi halisi za mataifa mbalimbali ambazo picha hubadilishwa kiutaalamu ili kufanana na mhusika. Pia wanauwezo mkubwa sana wa kujipenyeza na kuingia nchi yeyote na kufanikisha mauaji.

Katika mauaji wanayoyafanya pale mashariki ya kati, mtindo maarufu ni ule ya wauaji wakishambulia huku wakiwa wanatumia usafiri wa pikipiki. Mtindo huu ndio umetumika kuwaua maprofesa na wanasayansi wa nyuklia wanne wa Irani mpaka sasa. Katika mtindo huu, kawaida timu ya wauaji inakuwa na watu wanne

1.TRACER-huyu anamfatilia mlengwa anayetakiwa kuuawa

2.TRANSPOTER-huyu anaiongoza timu ya wauaji kwa mlengwa huyo anayetakiwa kuuawa

3.HELPER-huyu anaendesha pikipiki, anakuwa amembeba muuaji

4.KILLER-huyu ndio muuaji hasa, anafyatua risasi au kurusha magetic bomb kwa target(hili bomu linaweza kumuua mlengwa tu huku wengine wakijeruhiwa)

Unaambiwa huyu shooter anauwezo wa shoot accurately katika speed yeyote bila kupepesuka hata kidogo yani hakuna hata kutingishika akilenga mwendo kasi wowote ule bila kukosa au kurusha bomu likanasa katika sehemu ya gari anayotaka linase sehemu ambapo mara nyingi huwa ni upande wa gari aliokaa mlengwa na kitendo hiki huwa cha haraka sana kiasi wahusika huwa ngumu kutambua kama kuna kitu kimewekwa au kurushwa kwenye gari. Mtindo huu ndio 'Trade Mark' ya mauaji ya KIDON

haya ni machache katika yale machache,mengi kuhusu kitengo hiki. Kwa machache zaidi vitabu hivi ni vizuri; GIDEON'S SPIES: The inside story of Israel legendary secret service by Gordon Thomas na SPIES AGAINST ARMEGEDDON: Inside Israel's secret wars by Dan Raviv and Yossi Melman .
Vitabu viko hapo chini nime attach

Karibuni mwenye elimu zaidi kuhusu KIDON

 

Attachments

Oooh! My nation!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nasubiri kitabu.......nataka kujua mbinu zao mbalimbali.......
nimejaribu sana kuapload lakini inaiambia errors, ngoja niendelee kujaribu
 
Kama wanaweza kupokea vijana wawafundishe nafikiri tuwapeleke na sisi tuwe na hazina ktk jeshi letu.
 
Na mimi nataka nikajiunge huko maana hii nchi yetu kuna watu Wa kuwafanyia assassination wengi tu

wale wanapewa maelekezo wao wanatekeleza, ukijifanyia mambo yako unakuwa assasinated wewe mapema tu
 
Dah naomba uendelee kuna watu tunajifunza mengi sana. Hususani uzalendo kwa nchi yetu
 
Maisha yenyewe haya mafupi hivi unatuletea mambo ya Kidon. Usiku mwema

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk

hahaha, vipi kwani mkuu! Sasa si ndio vzr kuwa well informed. Haya usiku mwema na wewe pia
 
Na mimi nataka nikajiunge huko maana hii nchi yetu kuna watu Wa kuwafanyia assassination wengi tu

m ntakuwa nachukua mazoezi ya kuendesha pikipik kwa stlye za hatari.ukirud we m naajiriwa kama helper.mbona watakuwa waadilifu.no kuuza
wanyama,no kuweka pesa nnje,no kufisadi.kila mtu atakuwa muoga.chezea kuvumuzishwa kabla sir god mwenyewe ajaamua
 
Back
Top Bottom