Kidonda cha Usaha.

Majaribu2013

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
952
Reaction score
1,049
Watalaam nisaidieni,
wiki moja ilopita niliumia mguuni kwa kujikwaa kwenye ubao juu ya kisigino. kulionekana kama kubaki shimo, japo damu haikutoka sana na badala yake kama vimiminika vya mafuta viliendelea kutoka.
sasa kimekuwa kikifunga ukioga tu kinafunguka na juzi kimeanza kutoa usaha. ukilala ukiamka kimekauka fresh ukioga tu kinarudi upya, kumekuwa pia na maumivu makali kama kinajivuta lakini kikishajivuta baadae kinapasuka na usaha unatoka kama rangi ya damu, watu wananiambia ndo kinaelekea kupona,

je eti kitapona kwa style hii? nitumie dawa gani au nifanye kitu gani?
 
Ndugu Majaribu2013, jitahidi unapooga ufunge na karatasi laini ili maji yasikiguse kidonda, pili tafuta mu-aloe-vera na ukate jani lake kisha paka majimaji yake juu ya kidonda kutwa mara 2 kwa muda wa siku 4 mpaka 7 lazima kikauke.
 
Nenda hospitali ndg. au unataka kujitibu kwa mizizi? usichezee mwili wako namna hiyo, kwanza kwa nini kidonda ukitie maji wakati dawa za kuoshea zipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…