GE2025 Kiduku na Farida waachiwa kwa dhamana, wataendelea kuripoti polisi kila siku

GE2025 Kiduku na Farida waachiwa kwa dhamana, wataendelea kuripoti polisi kila siku

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wanaharakati wa mitandaoni, Innocent Paul Chuwa maarufu kama Kiduku, na Farida Mikoroti, waliokamatwa kwa tuhuma za makosa ya mtandao, wameachiwa kwa dhamana kutoka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Central Police) Dar es Salaam, Jumatano Oktoba 01, 2025.

Wawili hao wameshikiliwa kwa takribani juma moja tangu kukamatwa kwao, huku wakielezwa kuwa licha ya dhamana hiyo, watalazimika kuripoti kituoni kila siku asubuhi. Polisi pia wamesema kuwa muda wowote wanaweza kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mawakili waliokuwa mstari wa mbele kufuatilia dhamana hiyo ni Kulwa William Maduhu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania na Fredrick Msaki kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika. Wote walishirikiana kuhakikisha kuwa wanaharakati hao wanapewa haki zao kisheria katika mchakato mzima wa dhamana.

Pia Soma: GE2025 - Polisi: Paul Chuwa (Kiduku) tunamshikilia kwa tuhuma za makosa ya Kimtandao

G2LEVMDXUAAcAIs.jpg
 
Wanaharakati wa mitandaoni Innocent Paul Chuwa (Kiduku) na Farida Mikoroti muda mfupi uliopita leo, Jumatano Oktoba 01.2025 wameachiwa kwa dhamana kutoka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Central Police) Dar es Salaam walipokuwa wanashikiliwa takribani juma moja tangu walipokamatwa, wakituhumiwa kutenda makosa ya mtandao

Licha ya kwamba wamepatiwa dhamana, lakini sasa watalazimika kuripoti kituoni hapo kila siku asubuhi, ikielezwa kuwa muda wowote wanaweza kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili,

Mawakili Kulwa William Maduhu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania na Fredrick Msaki kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika ndio waliokuwa mstari wa mbele kufuatilia dhamana hiyo kwa muda wote huo.

Jambo TV itakuletea taarifa zaidi kuhusiana na hilo.
 
Back
Top Bottom