Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Jana, pale Mwanza bondia mtanzania Kiduku alipanda ulingoni kwa pambano la raundi 12 la ubingwa wa WBF. Alipambana na bondia Wellem wa Afrika ya Kusini.
Wellem, akitumia jab yake ya kushoto na urefu wake, alifanikiwa kumweka mbali Kiduku na kuvuna points za kutosha kumpatia ushindi wa jana. Wellem alikuwa mjanja katika kukwepa kukaribiana au kubananishwa kwenye kona na Kiduku.
Majaji wote watatu wakampa ushindi Wellem. Ushindi wa points nyingi kuliko alizopata Kiduku. Wellem, pamoja na kumpongeza Kiduku kwa kumpa pambano lenye changamoto, alijivunia kutojulikana kwake mtandaoni (kutokuwepo mapambano yake youtube).
Kimichezo, kiungwana na katika ukweli, Kiduku alisema kuwa Wellem ni bondia mzuri na yuko vizuri. Akasema amejifunza mengi kutoka kwa Wellem na anatarajia kupitia makocha wake atayafanyia kazi makosa yake ili kuwafurahisha watanzania wakati ujao.
Uungwana na ukweli ni asili ya watu wa Morogoro? Maana na Mandonga naye ni wa hukohuko😂😂