Kiduku ni mkweli na muungwana. Ni asili ya watu wa Morogoro?

Kiduku ni mkweli na muungwana. Ni asili ya watu wa Morogoro?

Jana, pale Mwanza bondia mtanzania Kiduku alipanda ulingoni kwa pambano la raundi 12 la ubingwa wa WBF. Alipambana na bondia Wellem wa Afrika ya Kusini.

Wellem, akitumia jab yake ya kushoto na urefu wake, alifanikiwa kumweka mbali Kiduku na kuvuna points za kutosha kumpatia ushindi wa jana. Wellem alikuwa mjanja katika kukwepa kukaribiana au kubananishwa kwenye kona na Kiduku.

Majaji wote watatu wakampa ushindi Wellem. Ushindi wa points nyingi kuliko alizopata Kiduku. Wellem, pamoja na kumpongeza Kiduku kwa kumpa pambano lenye changamoto, alijivunia kutojulikana kwake mtandaoni (kutokuwepo mapambano yake youtube).

Kimichezo, kiungwana na katika ukweli, Kiduku alisema kuwa Wellem ni bondia mzuri na yuko vizuri. Akasema amejifunza mengi kutoka kwa Wellem na anatarajia kupitia makocha wake atayafanyia kazi makosa yake ili kuwafurahisha watanzania wakati ujao.

Uungwana na ukweli ni asili ya watu wa Morogoro? Maana na Mandonga naye ni wa hukohuko😂😂
ukishakuwa na pesa za haki tabia za uungwana huwa karibu yako, ila ukipata zile pesa za mang'amung'amu amini nakwambia utakuwa mchungu kama piriton
 
Ile jab ya Wellem imenikumbusha pambano la Lenox Lewis na Mike Tyson. Lewis alimkaanga Tyson kwa jab. The jab gives distance, it explores the opponent, it makes the opponent busy muda wote na zaidi inalipa point. Hata hivyo majaji walikuwa fair sana kwa kiduku. Zile points alizo score sikuziona ktk ring. Halafu kiduku anapigana vizuri ila hana mbinu mbadala zaidi ya kumuweka opponent wake ktk Kona tuu Sasa atawapiga wa ndani lakini siyo kama yule jamaa.
Katika mabondia nilikua siwaelewi ni Lenox lewis,yaani anatumia Kono lake refu kumzuwia na kudokoa uso wa adui apate point
 
Mimi huwa nafikiria Kigoma ni mambo ya music Morogoro ndondi na Kilimanjaro biashara.

Ukioanisha watu walio kwenye hizo industry hapo utagundua hiyo mikoa ndiyo inayoongoza kwa vipaji hivyo.
Umesahau: pwani ngoma; kagera katerero; Tanga mahaba, rukwa uchawi, iringa na njombe ukimwi, Arusha bangi; mbeya ubonge nyanya, singida chini.
 
Back
Top Bottom