Kiemba mchambuzi bora asiyezungumzwa

Singasinga

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2011
Posts
2,711
Reaction score
3,279
Habari wakuu

Nimewasikia Kiemba na Shafih leo kwenye kipindi cha Sport Extra.
Asee Shafih ni mweupe kabisa kwa Kiemba.

Yani kuna muda Shafih alikua anatoa sababu za Namungo kufanya vibaya, Kiemba alikuja akachana chana kabisa kile alichokua ameongea Shafih,nadhan ata yeye aligundua kaongea utopolo kabisa.
Eti Namungo haifanyi vizuri sababu Kiongozi mkuu wa team yuko busy na siasa[emoji23]
 
Kiemba hajui kuongea vizuri alafu hajui kuchambua mpira kiundani yeye anachojua Ni kuongea ukweli tu Sio tofauti na hapo mchambuzi wa mpira hapa bongo ambaye anajua kuchambua mpira mpaka mwenyewe unafurahi na kuongezea kitu kichwani Ni GEORGE AMBANGILE tu
 
Ukishakuwa mchezaji mkubwa huwezi fananishwa na walioishia Umitashumta. Shaffih anajua mpira wa Google hajaucheza professionally.

Full stop.
Kabisa kaka eti anadai Namungo haifanyi vizuri sababu kiongozi wao yuko busy na mambo mengine ya kisiasa
 
Kwani ili uwe mchambuzi kamili vitu gani vya kuzingatiwa?
 
Nakuunga mkono,na bora mwngine Adam Ambangile wa Abood Fm Moro
 
Hapa kwa ambangile umenikosha haswaaa!!!
Kasoro mambo mambo yako ya diamond.😁
 
Hao Kina Shafi Dauda au Edo Kumwembe wanajua kuchambua siasa za mpira na kufanya uwakala wa wachezaji...lakini siyo kuchambua mpira kwenye pitch wanaachwa mbali sana.
 
Hao Kina Shafi Dauda au Edo Kumwembe wanajua kuchambua siasa za mpira na kufanya uwakala wa wachezaji...lakini siyo kuchambua mpira kwenye pitch wanaachwa mbali sana.
Kabisa kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…