Kifaa cha kupimia ukimwi

Christa

Member
Joined
Dec 15, 2012
Posts
37
Reaction score
4
Ni kweli kuna kifaa cha kujipimia HIV bila kwenda hospital? Kama kipo kinapatikana wapi na kinaitwaje?
 
Mkuu Christa,
kifaa/vifaa vipo ila pamoja na uwepo wake ni vizuri kupima katika kituo cha afya au hospitali.Hii ni kwa sababu;

1. Upimaji: Pamoja na kupatikana kwa vifaa, bado utahitaji Reagents, ambazo unaweza kupata zikiwa zimekwisha muda wake(yaani expired), hii huweza kuhatarisha majibu utakayoyapata.

2. Kupokea majibu bila ushauri nasaha: Watu mbalimbali hupokea majibu ya ugonjwa wa UKIMWI(HIV/AIDS) kwa njia tofauti tofauti. Hii hupelekea wengine kufanya maamuzi mabaya kwao wenyewe(mf. kujiua, kupata maambukizi mapya) au kwa watu wengine(mf Kueneza ugonjwa huu).

3. Maamuzi mara baada ya kupima: Kwa baadhi hawataona umuhimu wa kurudia kupima tena baada ya muda fulani (hasa wale ambao watakuta wana majibu mazuri) na wale wenye majibu yasiyo mazuri kufanya maamuzi yasiyo ya busara n.k

So pamoja na mengine mengi ni bora kupima sehemu husika hasa!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…