Mkuu Christa,
kifaa/vifaa vipo ila pamoja na uwepo wake ni vizuri kupima katika kituo cha afya au hospitali.Hii ni kwa sababu;
1. Upimaji: Pamoja na kupatikana kwa vifaa, bado utahitaji Reagents, ambazo unaweza kupata zikiwa zimekwisha muda wake(yaani expired), hii huweza kuhatarisha majibu utakayoyapata.
2. Kupokea majibu bila ushauri nasaha: Watu mbalimbali hupokea majibu ya ugonjwa wa UKIMWI(HIV/AIDS) kwa njia tofauti tofauti. Hii hupelekea wengine kufanya maamuzi mabaya kwao wenyewe(mf. kujiua, kupata maambukizi mapya) au kwa watu wengine(mf Kueneza ugonjwa huu).
3. Maamuzi mara baada ya kupima: Kwa baadhi hawataona umuhimu wa kurudia kupima tena baada ya muda fulani (hasa wale ambao watakuta wana majibu mazuri) na wale wenye majibu yasiyo mazuri kufanya maamuzi yasiyo ya busara n.k
So pamoja na mengine mengi ni bora kupima sehemu husika hasa!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.