Kifaa cha usikivu wa (masikioni)

Kifaa cha usikivu wa (masikioni)

Mkuu kama masikio ya mdogo wako yanapiga kelele sikushauli ununue mashine hizo maana utapoteza tu hela zako nina mdogo wangu alikuwa anasikia kama uyo wako ila masikio mdogo wangu anavyosema ni kuwa anasikia kelele masikioni tulimpeleka kupima wakadai anunue hizo machine tukanunua machine hizo laki saba alivyovaa machine kelele zikazidi ilibidi hasizitumie tena zile machine zina msaada kwa wale waliozaliwa hawasikii au wasio sikia kelele kwe masikio yao
Walisema chanzo cha kelele masikioni ni nini?
 
Inategemea na loss ya usikivu hizo mashine ni lazima zinunuliwe kwa kuonyesha vipimo ili wajue wanakupa mashine za aina gani.nenda muhimbili kuna jengo la richmond uliza hospital ya vifaa vya masikio utawaona na watakushauri aina gani ya kifaa ununue.nilishawahi kununua cha mtoto set kwa laki nane
 
Wadau habarini za asubuhi..naomba niende kwenye mada husika hapo juu..nina mdogo wang alikuwa mzima kabisa utotoni lakin kwa sasa hasikii baada ya kupima muhimbili wakatwambia kuwa hawezi kusikia tena ina bidi anunuliwe kifaa man ni mwanafunzi..kifaa chenyewe tumeenda kuuliza nauzwa milioni moja n la laki sita kwa vyote na kimoja sh..850000..naomba kupata msaada kama kuna namna yoyte ya kupata kifaa hicho kwa garama nafuu napenda nipate na ushauli katika hili jamani na mwanafunzi anajitaidi sna darasani na ni wa kike..japo nimesikia kifaa hicho kina kelele sna tunaweza kukipata na bado asikivae kwa kelele zake..naomba msaada wa mawazo katika hili kwa mwenye maarifa zaidi...ahsanten
Sikiliza nikwambie mimi ni mtumiaji mmojawapo wa kifaa hiko, hivyo vinauzwa kulingana na namba ya kifaa alichoandikiwa. Mimi mfano nilinunua kifaa cha shilingi 360000 kwa kimoja, viwili ni 720000. Ukiwa na tatizo kubwa unapewa namba kubwa zaidi, gharama pia inapanda.

Duka lake lipo Upanga ukiwa unafuata njia iendayo Muhimbili hospital kutoka makutano ya barabara jirani na shule ya msingi Muhimbili. Utakutana na njia panda jirani na Temple, ingia kulia hadi ufike jengo la Richmond tower. Hapo ulizia duka liitwalo Hear well, utaoneshwa.

Tahadhari(ukiona haina tija si lazima uichukue)
Vifaa vile haviondoi tatizo bali vinazidisha tatizo kama anao uwezo wa kusikia kidogo na si ubovu kabisa. Nakushauri usimwache akatumia, vinaharibu masikio. Vinavuta sauti kwa ulazima lakini siyo clear sound, halafu vinavuta kila aina ya sauti sehemu yenye sauti zaidi ya moja lazima atapata tabu.
 
Sawa hapo wanaita Asymmetric hearing loss!
Ila Hearing Aids ina msaada kidgo sana kwa walengwa
Ile mashine wakati mwengine sauti haieleweki!! Uko wapi nnazo mashine hizo mbili mapya kabisa nilipewa na Star key Foundation shirika la Marekani
Ukumbuke zina uwezo tofauti hizo mashine, ukimuuzia yenye uwezo mkubwa utamharibu kabisa. Hizo hutolewa kulingana na ripoti ya daktari, si kuuzwa kiholela. Hujui kaandikiwa akanunue mashine namba ngapi
 
kifaa chenyewe tumeenda kuuliza nauzwa milioni moja n la laki sita kwa vyote na kimoja sh..850000..naomba kupata msaada kama kuna namna yoyte ya kupata kifaa hicho kwa garama nafuu napenda nipate na ushauli katika hili jamani na mwanafunzi anajitaidi sna darasani na ni wa kike
Waweza kukiangalia hapa hicho kifaa: www .amazon.com au tafuta kwenye site nyingine (Ila iwe baada ya kupata mwongozo wa dakitari, na kujua namba sahihi) kisha wasiliana nami.

Na taratibu za kukifikisha nchini ziko hapa: www.bit.ly/101buy4me

Ukiagiza ghalama itakuwa ni ndogo mara dufu.

Karibu
 
Tahadhari(ukiona haina tija si lazima uichukue)
Vifaa vile haviondoi tatizo bali vinazidisha tatizo kama anao uwezo wa kusikia kidogo na si ubovu kabisa. Nakushauri usimwache akatumia, vinaharibu masikio. Vinavuta sauti kwa ulazima lakini siyo clear sound, halafu vinavuta kila aina ya sauti sehemu yenye sauti zaidi ya moja lazima atapata tabu.

Nina ukosefu wa kusikia sikio moja. Niliacha kuitumia hearing aid yangu na kuamua kulitegemea sikio hilo moja lililobaki kwasababu kwakweli hearing aid inakera sana. Inaleta sauti kubwa mno directly sikioni tena bila sense of direction. Sehemu ya kelele usipozima ni shida kubwa. Hata hivyo sehemu yenye utulivu kama darasani inafaa kwa kiasi kikubwa.

hearing aid.jpg
 
Kodi tu aangalie... Hawa TRA wa hapa bongo hawana dini mkuu. Mkiweza ku underdeclare value ya mzigo mtakuwa mmefanya la maana.
 
Nina ukosefu wa kusikia sikio moja. Niliacha kuitumia hearing aid yangu na kuamua kulitegemea sikio hilo moja lililobaki kwasababu kwakweli hearing aid inakera sana. Inaleta sauti kubwa mno directly sikioni tena bila sense of direction. Sehemu ya kelele usipozima ni shida kubwa. Hata hivyo sehemu yenye utulivu kama darasani inafaa kwa kiasi kikubwa.

View attachment 685681
Aisee hivyo vidude mimi nina matatizo masikio yote na vilinishinda, ukivaa muda mrefu kichwa kinauma. Sikio lenyewe linauma, ukivaa barabarani honi inapigwa mbali unahisi gari au pikipiki ipo nyuma yako.

Darasani ndiyo vinasaidia, ila akinong'ona mmoja au kukiwa hakuna utulivu nje ya eneo ulilopo ni kazi bure. Vinafanya kazi sehemu yenye ukimya mno, aisee mimi vimenishinda
 
Mimi pia kilinishinda kwa sababu hizo. Lakini angalau kilinisaidia kupunguza sauti ninapoongea. Najihisi naongea kwa sauti ndogo kutokana na tatizo la usikivu ila kumbe wanaonisikiliza wanahisi sauti iko juu sana.
 
Kwa hiyo mkuu kimekushinda kabisa..daa ngoja akapimwe tuone kama kitamsaidia..
 
Aisee hivyo vidude mimi nina matatizo masikio yote na vilinishinda, ukivaa muda mrefu kichwa kinauma. Sikio lenyewe linauma, ukivaa barabarani honi inapigwa mbali unahisi gari au pikipiki ipo nyuma yako.

Darasani ndiyo vinasaidia, ila akinong'ona mmoja au kukiwa hakuna utulivu nje ya eneo ulilopo ni kazi bure. Vinafanya kazi sehemu yenye ukimya mno, aisee mimi vimenishinda
Sas mkuu hapo ngoja tumnunulie tu atakuwa anavaa akishidwa ataviacha..mana dogo yuko vizur darasani
 
Kwa hiyo mkuu kimekushinda kabisa..daa ngoja akapimwe tuone kama kitamsaidia..
Kila la kheri mkuu. Ongea na Mwl.RCT kuangalia uwezekani wa kuagiza ili ukipate kwa bei ndogi zaidi. Kiuhalisia wafanyabiashara bongo huwa wanaongeza profit margin kubwa sana kwenye bei za bidhaa.
 
Sikiliza nikwambie mimi ni mtumiaji mmojawapo wa kifaa hiko, hivyo vinauzwa kulingana na namba ya kifaa alichoandikiwa. Mimi mfano nilinunua kifaa cha shilingi 360000 kwa kimoja, viwili ni 720000. Ukiwa na tatizo kubwa unapewa namba kubwa zaidi, gharama pia inapanda.

Duka lake lipo Upanga ukiwa unafuata njia iendayo Muhimbili hospital kutoka makutano ya barabara jirani na shule ya msingi Muhimbili. Utakutana na njia panda jirani na Temple, ingia kulia hadi ufike jengo la Richmond tower. Hapo ulizia duka liitwalo Hear well, utaoneshwa.

Tahadhari(ukiona haina tija si lazima uichukue)
Vifaa vile haviondoi tatizo bali vinazidisha tatizo kama anao uwezo wa kusikia kidogo na si ubovu kabisa. Nakushauri usimwache akatumia, vinaharibu masikio. Vinavuta sauti kwa ulazima lakini siyo clear sound, halafu vinavuta kila aina ya sauti sehemu yenye sauti zaidi ya moja lazima atapata tabu.
Ahsante sna mkuu..balikiwa sana..
 
Dah,imenisikitisha mno kwakweli.
Nakushauri nenda pale Shule ya Msingi Buguruni Viziwi watakusaidia,maana pale huwa mashirika na wafadhili mbali mbali hujitokeza mara nyingi sana hasa shirika la waamerika liitwalo Star Key hawa hujitolea kuwapima na kuwapa wahitaji hawa vifaa hivyo bure kabisa.
Nenda pale utapata ufafanuzi my kaka.
 
Ahsante sana dada,,,maisha ndio yanakwenda hivyo mdogo dada angu..jua mvua wakati mwingine vyote kwa pamoja..vyuma vyenyewe ndio hiv tena [emoji15]
 
Back
Top Bottom