Kifaa kinachoitwa Distributor

msimamia kucha

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Posts
683
Reaction score
551
Wakuu habari za Asubuhi. Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, naombeni kujuzwa na kuonyeshwa mahala hicho kifaa kilipo kwenye engine ya Gari a in a ya Spacio New Model Kama nilivyoambatanisha na picha ya engine maana mimi si mjuzi wa nagari.

Nawasilisha.

Yaani unaulizia Distributor kwenye 1NZ~FE?

Distributor nyingi zimeishia kwenye gari za early 90's.

Late 90's ikaja Wasted spark, yaani mfano unakuwa na ignition coils mbili ambapo kila coil moja inafeed cylinder mbili.

Early 2000 ndio zikaja hizi DIS kama hiyo yako. Distributorless Ignition System. Yaani kila cylinder inakuwa na coil yake.

Kama upo kijijini halafu fundi wako ndio amekupa habari za distributor, anza kukimbia kabla halijakukuta jambo.
 
Mkuu shukrani, ni kweli engine ni vvti sasa chuma haiwaki ilipigwa maji sana kuna fundi niliongea nae akadai itakuwa hiyo distributor.
Unaosha engine ya petrol na maji ili ugundue nini mkuu?....

Hapo matatizo mmeyachokonoa wenyewe.

Connectors za umeme ni nyingi kwenye hiyo engine sijui maji yayakuwa yameingia wapi. Anzeni kuchomoa connector moja moja muangalie.
 
Shukrani mkuu ndo mana nimekimbia kuja kupata maoni kabla sijafanya chochote.
 
Unaosha engine ya petrol na maji ili ugundue nini mkuu?....

Hapo matatizo mmeyachokonoa wenyewe.

Connectors za umeme ni nyingi kwenye hiyo engine sijui maji yayakuwa yameingia wapi. Anzeni kuchomoa connector moja moja muangalie.
Shukrani mkuu.
 
Kwahiyo mkuu, ishu itakuwa hizo connector kwa maana ni kuzichomoa Ku check kama zimeingia maji zikauke au zisafishwe.
 
Distributor iko kwenye generation ya nyuma ya hio engine yani A series engines. 4A, 5A, 7A!

Zilipoanza Z series wakahamia vvti wameachanaga na hizo mambo za distributors. 1NZ, 2NZ, 1ZZ, 2ZZ, 1AZ, 2AZ nk. Humu kuna coils tu hamna distributors.
 
Amenikumbusha injini ya 1S-U iko kwenye mark II GR. ina Distributor, enzi hizo sisi tunaita BIUSUBITA
 
Kwahiyo mkuu, ishu itakuwa hizo connector kwa maana ni kuzichomoa Ku check kama zimeingia maji zikauke au zisafishwe.
Majuzi hapa nilifanya kuosha gari kwa maji ya presha, kumbe baadhi yakaingia kwenye kompyuta ya power sterling, gari ina PS ya umeme, hayakukaushwa mapema yakawasha taa ya P/S kompyuta ikawa imekufa na sterling ikawa ngumu balaa, unatumia nguvu mno kulikatisha kona. Tulipoenda kusoma kwa DIAGNOSIS MACHINE, tukaja kugundua kuwa shida ni ECU ya P/S. Nachotaka kusema ni kuwa, maji kwenye engine ni hatari sana kwa gari hizi za umeme, kabla hujaanza kupangua vitu, tafuta mashine isome tatizo la gari lako ili utibu kitu sahihi.
 
Shukran mkuu
 
Ukitaka kukiona nenda kafungue Boneti ya land Rover 109 , starlet, Carina TI na SI zile za mwanzoni, Corolla za mwanzoni kabisa model za zamani. Humo haipo. Kilishakuwa replaced na vifaa vingine.
 
Kwahiyo mkuu, ishu itakuwa hizo connector kwa maana ni kuzichomoa Ku check kama zimeingia maji zikauke au zisafishwe.
Next time unapoosha engine hakikisha gari ipo idle yaani inaunguruma na engine ni ya moto ili kukausha maji jwa haraka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…