Kifaa kinachoitwa Distributor

Kifaa kinachoitwa Distributor

hicho kidude kipo kwenye engine Kama hii,mbele kidogo ya hose iliyounganishwa na chupa ya atf
IMG_20221026_194303_094.jpg
 
Unaosha engine ya petrol na maji ili ugundue nini mkuu?....

Hapo matatizo mmeyachokonoa wenyewe.

Connectors za umeme ni nyingi kwenye hiyo engine sijui maji yayakuwa yameingia wapi. Anzeni kuchomoa connector moja moja muangalie.
Ushamba hua Ni mzigo mkuu,sielewi hata hua wanataka engine ing'ae ili iweje sasa.
 
Next time unapoosha engine hakikisha gari ipo idle yaani inaunguruma na engine ni ya moto ili kukausha maji jwa haraka sana.
Kuosha engine Ni ujinga arifu, Hakuna Gari ambayo imeshawahi kupata matatizo kisa engine yake haijaoshwa lkn Kuna Gari nyingi sana zimeharibika sababu ya engine imeoshwa na maji.
 
Ushamba unatusumbua hapo kwenye injini mimi napulizaga na upepo wa presha bas vumbi likitoka imetosha ila mtu anataka injini iwake kama kioo wakati hata barabara zetu chafu tu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kuosha engine Ni ujinga arifu, Hakuna Gari ambayo imeshawahi kupata matatizo kisa engine yake haijaoshwa lkn Kuna Gari nyingi sana zimeharibika sababu ya engine imeoshwa na maji.
Kuna fluid yake inapuliziwa na ile mashine ya kuoshea gari ipo kama povu hivi ikishapita kila sehemu engine inatakata bila hata kusuguliwa inangaa kama mpya.

Nimetumia ipo vema sana na haina shida. Nitakupigia picha ya kopo yake uione maana na mimi nilipewa na mshikaji nikatafute. Nikipata nitaweka hapa duka wanapouza.
Screenshot_20221210_170120.jpg
 
Hapo ukute ni mdada hataki shida
Anakuuliza tu Kwani inauzwaga sh ngapi[emoji28][emoji28][emoji28]
Ishu ya kukausha tuu Engine iliyooshwa wahuni wanataka Maelfu hapo hapo kwani angeikausha si angepata chake kutokana na kazi ilivyo ndio maana life inakua ngumu kwa sababu ya watu kutokua waaminifu..
 
Mkuu shukrani, ni kweli engine ni vvti sasa chuma haiwaki ilipigwa maji sana kuna fundi niliongea nae akadai itakuwa hiyo distributor.
Fundi Maiko atakuharibia gari!

Kwanini unaosha engine ya gari kwa maji kwa hao waosha magari?

Engine ya gari uwe unaifuta mwenyewe kwa kitambaa chenye unyevu, kama kuna sehemu wanaosha kwa kutumia steam peleka lakini si kwa hizo njia za kienyeji.
 
Back
Top Bottom