Kifahamu kilimo cha maua

Maua yanahitaji ndege maalum yenye 'cold room' ambazo zinahitaji mzigo wa kutosha kutua kila siku. KIA hamna ndege hizo
 
Maua yanahitaji ndege maalum yenye 'cold room' ambazo zinahitaji mzigo wa kutosha kutua kila siku. KIA hamna ndege hizo
Unadhani ndege za mizigo ni kama magari yakubebea mchanga? embu Google kidogo kuusu ndege za mizigo
 
Ngosha kasema hakuna siri asyoijua hapa nchini. Kwa hiyo mleta mada ungeelekeza swali panapostahili.
 
KIA nighali zaidi ndo maana hata kwenye utalii wageni wengi hushukia nairobi na huletwa kwa 4x4 mpaka huku kwa kuanza safari

Mkuu, maua yanahitaji cold storage facility ili yaandaliwe kabla hayajapanda ndege. Je KIA wanayo hiyo facility? Na kama wanayo ni affordable? Isije ikawa ni very expensive that's why wanapeleka jkia.
 
Mkuu hata minofu ya samaki???
 

Haya mau nazani wengi wetu watakuwa wanajua yanalimwa kwa mapambo pembeni ya nyumba au uwanjani.

Haya maua yana kazi ziadi ya hiyo na hii kazi ya pili ndo yenye pesa.



UNAIJUA CARETONOID?
Hii ndo pigment inayo fanya yai liwe na kiini cha njano.


Sasa haya maua ya Marigold yana kiwango kikubwa sana cha Caretonoid na hulimwa sana kwa ajili ya kulishia kuku.

Makampuni yanayo zalisha vyakula vyakuku hutumia unga wa haya maua ili kuweza kuchanganya kwenye chakula cha kuku hasa layers.


Pia hutumika kwenye kuku wa nyama na kufanya ngozi kuwa ya njano.

Haya maua hulimwa sana kwa wingi na kukauswa na kuswagwa na kuuzwa kwa watengenezaji vyakula vya kuku.

Kwa Tanzania makampuni ya utengenezaji wa vyakula vya kuku huwa hawayanunui kwa sababu ya bei.

Unaweza lima haya mau na ukauzia makampuni au pia kama unafuga kuku hasa wa mayai basi unaweza lima haya mau.


NI PESA SANA
 
Yatakubali huku kwetu kwenye kichanga?? Na yanakubali kwenye hali gani ya hewa?
 
Niliyalima mpaka sasa sijalipwa wala siyatamani
Tena sitaki mtu anishawishi mana nilishawishika nikapoteza hela zangu
Uko wapi? ulilima yale mbegu? Kampuni za Arusha walikuwa wanawapatia wakulima mbegu wanalima na wanavuna mbegu. mim sizungumzii mbegu nazungumzia Maua.

Hizo za mbegu nazijua sana nimefanya sana kazi na hizo kampuni hasa Multflower ya Arusha na Kuna kampuni moja ya Dada mmoja wa Kizungu.
 
Niliyalima mpaka sasa sijalipwa wala siyatamani
Tena sitaki mtu anishawishi mana nilishawishika nikapoteza hela zangu
Zile kampuni za mbegu zinasumbua sana hasa kama huja meet vigezo vyao.

Hii Margold unavuna maua pekee na si mbegu na unayakausha then unayasaga kwenye mashine
 
Pia yanatumika kupunguza mashambulizi ya wadudu yakilimwa katikati ya mazao....JKT wanayatumia sana kuyalima bembeni ya bustani za cabbage etc
 
Haya maua niliyapanda sana kama urembo wa nyumba
 
Maelezo mazuri asante! Issue ni je soko liko wapi? Wengi wamekichukia kilimo kwa sababu hizo! Anaambiwa zao fulani zuri, lina pesa & demand kubwa analima! End of the day hajui solo liko wapi anaishia kukata mtaji wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…