Sizungumzii kwamba yupo hai au amekufa, hiyo siyo ishu hapa, nadhani hjaelewa uzi mzima. Kwanza kama alivyo kuwa Osama, alzarqawi, na pia kulikuwa na Albaghadad mwingine kabla ya huyu, wote walikuwa wanakufa na kufufuka, kwenye haijalishi kafa ua yupo hai, ninacho zungumzia hapa ni namna watu wenye akili ndogo wanavyo aminishwa kuwa kuna 'gaidi' mahali na ili tuweze kumdhibiti, tupe haki zako za privacy, toa sheria hii weka ile n,k wakati mwisho wa siku waathirika ni mimi na wewe, sababu hapakuwa na kitisho cha gaidi, bali kimetengenezwa ili kutuporoka haki zote. Mwisho wa siku gaidi ni wewe na mimi, sababu ndiyo wahanga wa sheria hizo.