Kuna siku tumeenda porini ndanindani maeneo ya pwani kukusanya mahindi,sasa tumefika sehemu kuna ka center hivi gari yetu tuliyokuwa nayo ikazingua halafu ilipozingulia ni nje ya nyumba fulani nzuri ina fremu nzuri nje na ndani kumepaki Hiace, hiyo ni saa 6 usiku! Ghafla akatoka mtu ndani ya nyumba ile akasalimia tukamuambia tatizo akasema haina shida iacheni hii gari hapa hakuna mtu yeyote atasumbua hapa ni nyumbani kwangu,hapo jamaa yupo bwiii kalewa hatari na kaja na Bluetooth speaker inapiga ngoma za mbele za miaka ya 80 za kina Roxette,Chaka Khan,Beach boys,Lionel Richie nk..Jamaa akatuambia tuingie ndani kama vipi tupumzike mpk kesho asubuhi maana ana uhakika kipindi hiki cha mavuno lodge iliyokuwa kijijini hapo imejaa hatari na hadi akapiga simu hapo Lodge akapewa majibu hapohapo,tukaingia ndani kwa jamaa hatujui wala hatumjui ni mshikaji tu ambaye anaonekana ana exposure na pesa zipo..Ndio story zikaanza jamaa anaelezea kuwa amerudi kutoka mjini amemuachia mke wake anayempenda kila kitu mjini,yeye kaacha kazi Kenya kaamua kuja atulie na stress kijijini ndio ana hiyo nyumba na fremu na Hiace na mashamba ndio vitega uchumi alivyoamua kuanzisha..Sababu ya maamuzi hayo ni ndoa,alimuamini sana mke wake lakini vitu alivyokuwa anamfanyia ilikuwa ni hatari hiyo ikafanya jamaa apoteze focus kabisa ajikite kwenye pombe na maisha yake yalibadilika kabisa,yaani ilifikia kipindi mwanamke anaingia nyumbani kwake anachukua nguo na viatu vyake anampelekea mchepuko na jamaa anadai hakuwahi kumfanyia lolote yule mwanamke,lakini alianza dharau,matusi,kufuja mali za familia na kumuhonga mchepuko ghafla tu.Jamaa akasema katika kitu ambacho hawez kumshauri mtu ni ndoa na alituuliza mmeoa tukajibu ndio akasema ombeeni sana muwe na amani na wenzi wenu,maisha yakija kubadilika upendo ukapungua hiki maumivu ya moyo ambayo huwa yanatokea huwa hayavumiliki..Kufupisha story Mwaka juzi jamaa alifariki akiwa amekaa sebuleni kwake kijijini alipokuwa anaishi