Kifo cha Dkt. Magufuli kuipasua CCM 2025

Mtetezi wa wanyongwe, wakati kila mradi mkubwa ulifanyika huko ukanda wa nyonyo
Jinga mkubwa wewe, miradi ya mafuta Ohima to Tanga, Miradi ya SGR & umeme Rufiji, Njia nane ubungo to kibaha, ujenzi wa vituo vya afya, uboreshaji wa bandari, meli kwenye maziwa makuu, uboreshaji wa viwanja vya ndege, barabara, ujenzi wa stendi kila mikoa na (w) n.k, halafu unaandika ujinga hapa
 
Umetema madini kiongozi🙏🙏🙏
 
By all fairness, CCM kama chama kilikufa wakati wa JK. Ndio maana upatikanaji wa JPM kama mgombea wao iliacha maswali mengi. JK alishakiri kwamba yeye ndie alienda kikaoni na jina la JPM mfukoni. Rejea hotuba yake wakati wa mazishi ya JPM akijinasua na hearsay kwamba hakuwa anampenda JPM. Kwa maneno mengine hata huko CCM ndani ni one man show wakitumia ubovu wa Katiba kwamba rais ni mungu mtu na akiwa chamani kwake pia ni rais. Ndani ya CCM Mwenyekiti (rais na amirijeshi) amtakaye huwa. Kinachofuata ni matumizi ya dola na vyombo vyote kuibakisha madarakani.

Kama huamini kama CCM imekufa au ni ya watu wachache, itisheni uchaguzi usimamiwe ki huru na haki utaona maajabu! Kwa ubunge watapata less than 40%. 60% watagawana ACT wazazendo 10% na CHADEMA 50%. Hata kwa urais hali ni hiyo hiyo hata CCM wamweke nani. Hata hao wanachama 8m wa CCM ni nadharia tu lakini ki uhalisia hawapo. CCM ilishakufa na wenyewe wanajua. JPM na sarakasi zake zote hakuwa mwumini wa chama chake ndio maana hakuwa na impact yoyote zaidi ya kutumia pesa za serikali atakavyo, tena kibaguzi akijifunika ngozi ya CCM. CCM imekufa its just a matter of time tutaambiwa mazishi na matanga yake kana KANU na cha mzee Keneth Kaunda, Banda Malawi na ZANU. Stay tuned!
 
1. CCM haina nguvu zaidi ya upinzani

2. Upinzani dhaifu ndiyo ...

Unaelewa ulichoandika?
CCM haina nguvu zaidi ya upinzani. Kimsingi, upinzani dhaifu ndiyo umeifanya CCM kuendelea kuwa madarakani pamoja na uchakavu na ukale wake bila kusahau kukosa mwelekeo, ufisadi na umalaya wa kisiasa.
c
 
Ccm ilishakufa hata magu bila police asingepita.Ccm hawana mtu anaeuzika kwa sasa,njia nyeupe kwa upinzani kama wwkijipanga.
Bora tumpe Rungwe kuliko ccm shamba la bibj
 
Huyu huyu ambaye alizuia ajira za wanetu kwa miaka 6!
Aliye zuia kupanda mishahara na madaraja ya watumishi!!
Labda mi sielewi maana ya kutetea wanyonge
 
Hata ikigawanyika - bila Tume huru ya Uchaguzi hakuna kipya ni kupoteza muda tu.
 
Magufuli kwa sasa ni kiongozi wa Malaika
 

Hakiyamungu angeendelea kuishi mpaka sasa watanzania tungeokota makopo mana alikuwa hajali kabisa ustawi wa watu yeye ilikuwa barabara tu.

Waliokuwa wanampenda jama ni wale ambao tayari wako ajirani au wana ajira na wenyewe walikuwa wanampenda kama kasumba ya mtanzani kwamba akishapata hataki mtu mwingine apate ili uzidi kumnyenyekea yeye. Kundi lingine lililokuwa linampenda ni lile la waliokuwa wanashangilia ili aliyefukuzwa afanane nao ili wote wote wawe maskini mana alijidai sana.

Kundi la tatu ni ambalo halina elimu kabisa kwa hiyo halijui hta future mana yake nini kinachokuja mbele yao sawa tu vyote maisha.

Kiujumla jpm angekuwa anaongoza nchi watu wangezidi kutembea uchi kwa kuchanganyikiwa
 
Elezea miradi aliyoifanya chato ni mingapi, kilimanjaro mingapi, arusha mingapi, ruvuma mingapi, mbeya mingapi?mwanza mingapi,
Yule alikua mbinafsi sana hata teuzi nyingi ni sukuma tu
Hao wasiokuwa wabinafsi wameitendea nini tanzania zaidi ya kuiba na kuingia mikataba ya kinyonyaji huku wakipeana nafasi za uteuzi za kujuana na kushindwa hata kutumbuana mtu akiharibu?

Ukitoa siasa zenu taka hakuna mahali ambapo magufuli hakupagusa kwa ukubwa au udogo. Iwe miundombinu ya umeme, iwe zahanati, vituo vya afya au hospital za rufaa, iwe miundombinu ya maji, iwe shule, iwe vivuko na meli, iwe barabara au viwanja vya ndege, iwe utoaji wa huduma bila rushwa katika taasisi za serikali..wasiotaka siasa za kijinga wanatambua mchango wa magu kwa nchi.
 
Mtetezi wa wanyongwe, wakati kila mradi mkubwa ulifanyika huko ukanda wa nyonyo
Huijui tanzania eng. Mzima unasikiliza story za vijiweni ,ungetembelea mikoa yote ya tz ndo ungejua nchi inajengwa namna gani ma hayati jpm.
 
Yawezekana pia yasingefanyika mauaji ungekufa wewe, waulize wakazi wa kibiti wanajua hili.

Uhuru usio na mipaka ni vurugu ndio maana wewe kama unaishi na wazazi wako huwezi kupita na demu sebuleni walipokaa wazazi wako ukaingia nae chumbani kumkaza. Au huwezi kukubali binti yako akupite sebuleni ulipokaa aingie chumbani na jamaa yake kukazwa japo ni sehemu ya uhuru.

Huwezi kujiona mjanja sababu kuna mtu usiyempenda amekufa wakati hata ndugu zako unaowapenda wamekufa na wataendelea kufa. Yawezekana hapo huna wazazi au mmojawapo alishakufa.
 
Yaani kwa umri wako bado unategemea kuajiriwa, bora Magufuli aliwafungiua watu wakajiajiri na amewaacha vizuri, isipokuwa wewe unayesubiri kuajiriwa
 
hebu tuambie kanda ya kaskazin alifanya nini.

e
Tulijua tu mtalalamika mlijifanya nchi ya kwenu tangu 1960, sasa cha moto mtakiona mlizoea kutumia rasilimali za nchi kuwekeza kwenu. Mna tofauti gani na aliyofanya magufuli, mnalalamika kwa kuwa magufuli aliwatemesha tonge. Na hamtalipata tena
 
Katb mpya inaweza kuwasaidia mcc katk pto lao linalokuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…