Kifo cha huyu jamaa kimenishtua, kimeniumiza, kimenifunza

Lighton

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
1,424
Reaction score
2,333
Habar za mchana wanajamvi.

Leo asubuhi nimepokea taarifa za kifo cha kijana mwenzetu. Ni mshkaji flan mpambanaji, ni mjasiriamali mwenye weledi, alipotoka mpaka alipofika inaelezea uhalisia wake wa upambanaji. Jamaa ni mtaratibu sana, ukiachana na kumfaham Kwa ukaribu, niliwahi kumsikia mke wake akiliongelea Hilo.

Ilifikia Hatua jamaa alikuwa anasahau madeni makubwa ambayo alikuwa anawadai watu, kwaajili ya utu tu.

Amefariki usiku wa kuamkia Leo, Juzi na Jana alikuwa na afya yake tu nzuri, ameshiriki chakula cha jioni na mke wake pamoja na watoto wake, na walipoenda kulala, mke na watoto wake ndiyo walio amka, jamaa yeye hakuweza kuamka Tena.

Ameacha mke, na watoto wawili, mmoja wa miaka 5 na mmoja wa miezi kadhaa.

Rip.
 
Apumzike kwa amani
 
Kifo hakiepukiki, uwe mpore au mgaidi,uwe mrefu au mfupi,uwe mzungu au mweusi,uwe mwanamke au mwanaume,kikombe lazima ukinywe. APUMZIKE KWA AMANI kijana mpambanaji, familia,jamii na taifa kwa ujumla tumepoteza nguvu kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…